Michezo

Mchezo ya Pamba Fc dhidi ya Dodoma Fm ni sawa na mgeni njoo mwenyeji apone

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Ule usemi wa mgeni njoo mwenyeji apone umetimia kwa timu ya Pamba FC ya Jijini Mwanza kutoa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Dodoma Fc, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza inaoendelea nchini.

Mchezo huo ulichezwa jana kwenye uwanja wa kisasa wa  Nyamagana ambapo Pamba FC ilifunga goli la pekee  ambalo limerudisha matumaini kwa wapenzi wa timu hiyo na wadau wa  soka mkoa wa  Mwanza kupitia kwa mchezaji Amos Mnyapi dakika ya 49.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Pamba FC Venance Kazungu alisema ataendelea kupambana kwa nguvu zake kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri na kwamba wachezaji wakimsikiliza watafika mbali na mashabiki wawe na imani na waiunge mkono.

Kwa upande wake Kocha Wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo alisema mchezo ulikua na ushindani, na wapinzani wao wamepata nafasi moja ambayo wameitumia vizuri na kupata ushindi, hivyo wanajipanga kufanya vizuri michezo ijayo.

Pia alisema mpira wa miguu una matokeo matatu ambayo ni kufunga, sare na kufungwa hivyo wao si malaika kila siku wafunge maana wote wanamuomba Mungu ndio ambaye kwenye mchezo huo kawapa wenzao nafasi ya ushindi kama ilivyo kwa misiba leo hapa kesho kule.

Naye Mwenyekiti wa MZFA, Vedastus Lufano ambaye alishuhudia mchezo huo alisema timu ya Pamba FC inatakiwa kupambana ili angalau ipate pointi kuanzia 12 na kwamba timu za Mwanza ni  nzuri kwani ligi daraja la kwanza ni  ngumu duniani kote maana kila timu inakuwa inataka kupanda ligi kuu, hivyo wanamwanza wanatakiwa kuziunga mkono timu zao zote.

Recommended for you