Audio & Video

MCHUNGAJI KULOLA SIYO WA MCHEZO MCHEZO

on

Na George Binagi-GBPazzo

Julai 23 hadi jana 30,2017 ulifanyika Mkutano wa Injili ulioandaliwa na Makanisa ya EAGT Kanda ya Kusini Jijini Mwanza.

Mhubiri aliyealikwa kuhudumu kwenye mkutano huo alikuwa Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani juu).

Katika Mahubiri yake, Dkt.Kulola alikuwa akisisitiza zaidi jumbe zenye lengo la kubadili fikra za wanadamu na siyo kuwapotosha kama ambavyo baadhi ya wahubiri wamekuwa wakiwahadaa waumini wao. BONYEZA HAPO CHINI KUSIKILIZA MANENO KUNTU YA MCHUNGAJI KULOLA.

Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Dkt.Daniel Moses Kulola akihubiri kwenye mkutano wa Injili ulioandaliwa na Makanisa ya EAGT Kanda ya Kusini Jijini Mwanza. Mkutano huo ulianza Julai 23 hadi 30 mwaka huu katika uwanja wa shule ya Msingi Buhongwa.

Mchungaji Mercy Kulola (Mama Mchungaji Daniel Kulola) akiwa kwenye mkutano huo

Viongozi mbalimbali wa dini wakihudumu kwenye mkutano huo ikiwemo kuombea wahitaji

Viongozi na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo

Watumishi mbalimbali wa Mungu

Baadhi ya watumishi wa Mungu walioshiriki mkutano huo

Baadhi ya watumishi wa Mungu walioshiriki mkutano huo

Baadhi ya watumishi wa Mungu walioshiriki mkutano huo

Mwimbaji wa nyimbo za injili akihudumu kwenye mkutano huo

Baadhi ya waliohudhuria mkutano huo ambao kwaya mbalimbali ikwemo Havillah Gospel Singers kutoka EAGT Lumala Mpya walihudumu. Bonyeza HAPA kwa habari zaidi.

 

Recommended for you