Audio & Video

Misungwi wajipanga wananchi kunufaika na huduma bora za afya

on

George Binagi-GB Pazzo, BMG

Waganga wafawidhi pamoja na wenyeviti wa kamati za afya katika halmashauri ya wilaya Misungwi mkoani Mwanza, wametakiwa kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF iliyoboreshwa ili kupata huduma bora za afya.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Eliurd Mwaiteleke aliyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waganga wafawidhi wa vituo vya afya na zahanati yaliyoshirikisha pia wahasibu pamoja na wenyeviti wa kamati za afya.

Mratibu wa mfuko wa CHF wilayani Misungwi, Azizah Mangu alisema washiriki 175 wamejewa uwezo kwenye mafunzo hayo kuhusu mfumo wa komputa wa FFARS kwa ajili ya utunzaji wa kumbukumbu za kifedha pamoja na CHF iliyoboreshwa ambapo kila Kaya yenye wategemezi sita itakuwa inachangia shilingi 30,000 na kupata huduma hadi ngazi ya rufaa kwa mwaka mzima.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke (kushot), akifungua mafunzo hayo. Waliokaa ni Mratibu wa mfuko wa CHF wilayani Misungwi, Azizah Mangu (kushoto) pamoja na Afisa mipango Misungwi Sylvia Rwehabura (katikati).

Mratibu wa mfuko wa CHF wilayani Misungwi, Azizah Mangu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.

Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wilayani Misungwi Dr.John Nyorobi pamoja na washiriki wa mafunzo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mwezeshaji Itendele Maduhu.

Mwezeshaji Itendele Maduhu akifafanua jambo kuhusu mfumo wa komputa wa FFARS unaotumika kwa utunzaji wa kumbukumbu za kifedha.

Mwezeshaji Abubakar Abdalla akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji.

Baadhi ya watendaji na wawezeshaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika kumbi tatu ambazo ni Graceland Hotel, CCM wilaya ya Misungwi pamoja na Kanisa Katoliki Misungwi.

Tazama video kwa undani zaidi wa habari.

Bonyeza BMG kwa habari zaidi.

Recommended for you