Habari Picha

Mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakabidhi Maktaba ya Kisasa Nyang’hwale mkoani Geita

on

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu, Bernedict Busunzu akipatiwa maelezo na mkurugenzi wa Read International, Bi Magdalena George wakati walipokuwa wakitembelea maktaba ya jamii ambayo hipo wilayani Nyang’hwale, katikakati ni katibu tawala wa Wilaya hiyo Fabian Sospeter.

Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu akikata utepe na katibu tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale Bw,Fabian Sospeter wakati wa zoezi la kukabidhi maktaba hiyo.

 

Sehemu ya vitabu ndani ya maktaba ya jamii wilayani Humo.

 

Sehemu ya vitabu ndani ya maktaba ya jamii wilayani Humo.

 

Meneja Ufanisi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu,Bw Elias Kasititila akielezea namna ambavyo wameguswa kuchangia maktaba hiyo.

 

Bi,Vannesa Kasoga akisoma taarifa ya ukamilikaji wa maktaba hiyo tangu ilipoanza kufanyiwa maboresho na kampuni ya ACACIA.

 

Mkurugenzi wa Read International ,Bi Magdalena George akielezea namna ambavyo wameweza kufanukisha kuhakikisha maktaba inakuwa kwenye muonekano bora.

 

Katibu tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale Bw,Fabian Sospeter akiwasisitiza wananchi pamoja na wanafunzi kutumia maktaba hiyo kujifunza mambo mbali mbali.
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wakati wa zoezi la kukabidhi na kuzindua maktaba ya jamii wilayani Nyang’hwale.
Wananchi ambao wamejitokeza kwenye zoezi la uzinduzi wa Maktaba.

 

Wanafunzi wa shule ya Msingi Karumwa wakiwa kwenye uzinduzi wa maktaba ya jamii.

Na Joel Maduka

Mgodi wa acacia Bulyanhulu kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la  read international wamekabidhi maktaba ya kisasa ya jamii ambayo imetumia kiasi cha sh,milioni 23  hadi kukamilika kwake  kwa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale ambayo itawasaidia wananchi kupata maarifa na kujifunza mambo mbali mbali kutokana na vitabu ambavyo vinapatikana.

Akizungumza jana wakati wa shughuli ya kukabidhi  wa maktaba ya jamii, Meneja Mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu alisema kuwa wanaamini katika kufikia Tanzania ya viwanda basi ni vyema watu wakawa na ufahamu ambao utawasaidia kujua fursa mbali mbali ambazo zinawazunguka hivyo kupitia maktaba hiyo wananchi wanaweza kusoma vitabu ambavyo vitawasaidia kujua mambo mbali mbali.

“Tunatambua umuhimu wa elimu na tunaimani kuwa jamii ya Wilayah ii itatumia vyema Maktaba hii kwa kusoma na pia kujifunza mambo mbali mbali ambayo yamo kwenye vitabu ambavyo vipo kwenye maktaba hii hivyo tunaomba iweze kutunza kama vile sisi tulivyoikabidhi ikiwa katika hali nzuri”Alisema Busunzu.

Hata hivyo kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya Hiyo Fabian Sospeter  aliwataka  wananchi pamoja na wanafunzi kujenga desturi ya kupenda kusoma vitabu  mara kwa mara na kwamba kufanya hivyo wataweza kujua mambo mengi zaidi.

“Wananchi niwasisitize kutumia maktaba hii kujifunza na kusoma masuala mbali mbali na ndani ya maktaba hii kuna vitabu vya kilimo ambavyo vitawasaidia wakulima kulima kilimo cha kisasa na ambacho kitawaletea faida”Alisema Fabian

Mabura Makonga na Georgi John walisema kuwa wanaamini kuwa maktaba hiyo itawasaidia kujua mambo mbali mbali huku wakishauri elimu itolewa zaidi kwa wananchi kutambua umuhimu wa kujenga  tabia ya kupenda kujisomea kwani wengi wao awana elimu na jambo hilo ni geni kwenye Wilaya hiyo.

Hata hivyo Bi,Vannesa Kasoga ameelezea uhaba ambao wanao kwenye maktaba hiyo kuwa ni  upungufu wa kompyuta saba,mashine ya kuzalisha nakala na upungufu wa baadhi ya vitabu.

Recommended for you