Audio & Video

MWANZA: Mshindi wa Vodacom M-Pesa akabidhiwa gari

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wateja Vodacom nchini wameanza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo fedha na gari kupitia kampeni ya miaka 10 ya M-Pesa ambapo hii leo Jijini Mwanza Bi.Pasquiner Karol Ignas amekabidhiwa gari aina ya Renault Kwid yenye thamani ya shilingi Milioni 25.

Hafla ya kukabidhi zawadi hizo imeambatana na sherehe za miaka 10 tangu kuanzishwa huduma ya M-Pesa, iliyofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rosalynn Mworia ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Vodacom Tanzania amesema huduma ya M-Pesa ilianza nchini mwaka 2008 na hadi sasa ina watumiaji zaidi ya Milioni nane huku ikichangia asilimia 37 ya pato la taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella ameipongeza kampuni ya Vodacom kupitia huduma ya M-Pesa kwa kuchangia ukuaji wa pato la taifa huku ikirahishisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo kufanya malipo ya umeme na maji.

Naye mshindi wa zawadi ya gari, Pasquiner Karol Ignas ambaye Muuguzi wa Afya katika Kituo cha Afya Nyankumbu mkoani Geita, ameshindwa kuzuia hisia zake kwa furaha na kububujikwa na machozi, amewasihi watanzania kutumia huduma za Vodacom ikiwemo M-Pesa ambapo wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kama alivyoshinda.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia), akimkabidhi mshindi wa nambari ya gari alilojishindia kupitia huduma ya M-Pesa

Kushoto ni mme wa Pasquiner Karol Ignas, mshindi wa gari kupitia kampeni ya M-Pesa

Pasquiner Karol Ignas (katikati) akifurahia baada ya kukabidhiwa funguo ya gari. Kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella na kushoto ni Rosalynn Mworia ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Vodacom Tanzania

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo

Rosalynn Mworia ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Vodacom Tanzania akizungumza kwenye hafla hiyo

Domician Mkama ambaye Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji, Vodacom Tanzania akizungumza kwenye hafla hiyo

Wakala Yohana Mahago akipokea cheti cha ufanisi

Wakala wa M-Pesa James Rwekaza akipokea cheti cha ufanisi wa kazi

Wakala wa M-Pesa Hosea Mashimba akipokea cheti cha ufanisi

Wakala Vedastus Lufano amejishindia shilingi Milioni moja kupitia huduma ya M-Pesa

Wakala Agnes Mazoya Manumbu amejishindia shilingi Milioni moja kupitia huduma ya M-Pesa

SOMA Kampuni ya Vodacom yaja kivingine

Recommended for you