Michezo

RC Mnyeti kuzindua michuano ya Chem Chem Cup 2018

on

Na Mwandishi Maalum, Manyara

Jumla ya timu 20, zinatarajiwa kushiriki ligi ya Chem Chem CUP, wilayani Babati mkoa wa Manyara ambapo zawadi zenye thamani ya sh 4.5 milioni zitatolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa ligi hiyo ambayo hufanyika kila mwaka,katika uwanja wa Mdori, Charles Godluck alisema, lengo lake ni kupiga vita ujangili na kuhamamisha  jamii uhifadhi za mazingira.

Godluck alisema, ligi ya chem chem CUP,mwaka huu inatarajwa kufunguliwa na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, Agosti 19 na itatanguliwa na mkutano wa kutolewa jezi wa timu zote agosti 10 mwaka huu.

“hivi sasa tumezitaka timu zote ifikapo Agosti 4 ziwe zimethibitisha lakini pia kujitokeza kwenye kikao cha kupanga ratiba Agosti 10″alisema.

Alisema mwaka huu bingwa wa soka, atapewa zawadi ya fedha taslimu 1.7 milioni na kombe,mshindi wa pili fedha 1.1 milioni, wa tatu 600.000 na wa nne 300,000.

“pia kutakuwa na zawadi wa kocha, bora, timu bora na mchezaji bora”alisema

Alisema katika michuano hiyo, pia kutakuwa na michezo kwa wasichana ambapo, bingwa atazawadiwa 400,000 na pia kutakuwa na ngoma za kitamaduni na michezo mingine.

Meneja wa taasisi ya Chemchem Foundation, Recardo Tossi, ambao wamewekeza ujenzi wa hoteli katika eneo la Mdori, alisema ligi hiyo, imekuwa ikishirikisha zaidi ya wanamichezi 400 na kuwa na ufanisi mkubwa.

“tunataka jamii ambayo inazunguka kijiji cha Mdori na tarafa nzima ya Mbugwe na wilaya ya babati, kuwa wahifadhi wazuri na kupiga vita ujangili”alisema.

Na hapa chini ni baadhi ya matukio katika picha ya michuano iliyofanyika mwaka jana ambapo timu ya Mdori fc ilijinyakulia kombe la michuano hiyo.

Recommended for you