Michezo

MICHUANO YA NDONDO CUP 2017 JIJINI MWANZA YAFIKIA PATAMU.

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Katika kukamilisha raundi ya tatu hatua ya makundi katika mashindano ya Ndondo Cup 2017 yanayotimua vumbi uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, timu ya Nyegezi Terminal imeilaza Igoma Heroes goli 4-1.

Mchezo ambao ulikutanisha timu zote kutoka kundi B,ambapo Nyegezi Terminal ilifunga goli kupitia washambuliaji wake Chika Chukwu dakika ya 13, Ayubu Suleiman dakika ya 22, Charles Msuka dakika ya 50 na Twalibu Ally dakika ya 52 huku Igoma Heroes wakipata goli kupitia kwa Bosco Kakoko dakika ya 56.

Chika Chukwu ndio aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo,na kijinyakulia kitita cha shilingi 30000 kutoka kwa HASFU Barber  Shop and SPA.

Chukwu alisema, amefurahia ushindi huo ambao umetokana na utayari wa wachezaji,hivyo wanasubilia mchezo wa Buzuruga Terminal na Mabatini Star ambapo utaamua kama wataweza kufuzu kuingia robo fainali.

Kwa upande wake Kocha wa Nyegezi Terminal Ibrahim Mlumba  amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa mchezo waliouonyesha,maana walikua kama wanaanza ligi,hivyo anaamini wakipata nafasi ya kuingia robo fainali watachukua ubingwa.

Hata hivyo katika mchezo huo, mchezaji wa Igoma Heroes Laurent Tumaini alipewa kadi nyekundu dakika ya 88.

Katika mchezo mwingine Copco Fc ili ibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya VIVA Fc,ambapo walifunga magoli kupitia washambuliaji Mohamed Sued dakika ya 32,Juma Nyange dakika ya 41 na 74 huku David Brandy akifunga dakika ya 84.

Recommended for you