Habari Picha

Michuano ya Rock City Cup 2018 kuanza kutimua vumbi Uwanja wa Nyamagana

on

Judith Ferdinand, BMG Habari

Mashindano ya Rock City Cup 2018 mkoani hapa yanatarajia kuanza kutimua vumbi Aprili  16,2018 katika uwanja mkongwe na wakisasa wa Nyamagana Jijini Mwanza.

Mashindano hayo yanatarajia kushirikisha timu 16 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza ambayo yamelenga kuchipua,kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana katika soka.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa  Kamati  ya Maandalizi ya Mashindano hayo Fabian Fanuel wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Fanuel amesema lengo la mashindano hayo ni kuchipua vipaji,kuhimiza uzalendo kwa wananchi kupenda kushabikia timu za nyumbani, kurudisha mshikamano na umoja pamoja na kuhamasisha kwenda viwanjani.

Amesema kwa mwaka huu wanaanzia mkoani Mwanza na Mungu akiwajalia miaka ijayo wataenda katika mikoa mingine kwani lengo ni kuendeleza soka nchini.

Pia amewaomba wananchi kujitokeza uwanjani na kuacha kuangalia mpira kwenye televisheni, kwani wanapotoa pesa kwa ajili ya kiingilio wanakuwa wanasaidia timu na wachezaji kupata mahitaji mbalimbali na kusonga mbele.

Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Mashindano ya MZFA, Kessy Mziray amesema wamekubaliana na mawazo ya waandaaji, hivyo usajili wa timu utaanza kuanzia  aprili 10 hadi 13 kwa na klabu yoyote inaruhusiwa kushiriki endapo inauwezo wa kugharamia wachezaji.

Mziray alisema gharama ya fomu ni 150000, timu 16 ndio zitakazo sajiliwa na kushiriki katika mashindano hayo kwa msimu huu.

Pia amesema klabu itaweza kumchezesha mchezaji yoyote ila tu asiwe amecheza kwenye timu inayoshiriki mashindano hayo mfano mechi ya kwanza alicheza huyu nyingine akachezeshwa mwingine hivyo aliwataka viongozi wa klabu hizo zitakazoshiriki kuwa wakweli katika usajili.

Hata hivyo alisema mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha shilingi  milioni 1.5, wa pili milioni moja, wa tatu laki tano, mchezaji bora ataondoka na fedha taslimu laki mbili na nusu.

Pia amesema watatoa zawadi kwa kipa bora, kocha bora, muamuzi bora, mfungaji bora ya shilingi laki mbili na nusu kwa kila mmoja, pia timu yenye nidhamu itajinyakulia  shilingi laki tano pamoja na kikundi bora chenye hamasa kitaondoka na shilingi laki tano.

Ameomba viongozi wa klabu watoe kwanza fursa kwa vijana waje kuonyesha uwezo na vipaji  vyao uwanjani kwani  lengo ni kuendeleza mpira wa miguu. Soma zaidi HAPA

Recommended for you