Habari Picha

“MIMI NDIE MSANII PEKEE WA HIP HOP AMBAE HATA P.FUNK MAJANI ANANIKUBALI”. ANASEMA NATTY E MKALI KUTOKA JIJINI MWANZA AMBAE ANAKUJA NA UJIO WA ALARM AKIWA NAE ILLUMINATION.

on

Alarm ndio Ujio Mpya wa Natty E (kushoto), na Illuminata (kulia).

Nadhani utakuwa unamkumbuka msanii Natty E halisi kama Edna Elisha ambae anasema kwa mara ya kwanza aliufanya Mtima wa Muandaaji wa Hit Songs mbalimbali hapa Bongo P.Funk Majani kumkubali kupitia ngoma yake ya Vuta Taswira aliyofanya na Kalla Jeremiah, kama unamkumbuka basi jiandae kwa ujio wake mpya akiwa nae Illuminata katika ngoma inayofahamika kama Alarm.

“Ukweli ni kwamba mimi ni msanii wa kike wa pekee ambae nilitokea kukubalika kwa P.Funk Majani baada ya kusikiliza wimbo wangu unaofahamika kama Vuta Taswira niliofanya na Kalla Jeremiah, Heshima pekee ambayo nataka kumpa kutokana na kuikubali kazi yangu ni mimi kufanya nae kazi, na nitakaza kama kawaida yangu” Alisema Natty E huku akibainisha kuwa kabla hajafanya kazi na P.Funk anataka kuufahamisha ulimwengu kuwa yeye ni level zingine kupitia wimbo wake ujao unaofahamika kwa jina la Alarm.

Vuta Taswira ni ngoma ambayo ilimpa shavu la kupata ma-air time ya kutosha kwenye Tv na Radio mbalimbali hapa nchini, ikifuatiwa na hits kama Hainaga Noma ambayo inakimbiza mbaya kwa sasa huku akiwa amesimama peke, lakini hapo awali alitamba na ngoma kama Mpango Mzima na Dunia Mapito aliyofanya na Sajna na nyinginezo nyingi.

Habari ya Tanzania kwa hivi sasa ni juu ya Ujio wa mwanadada huyu Natty E ambao unakwenda kwa jina la Alarm akiwa amefanya na mwana dada Illuminata kutoka Jijini Dar, ngoma ambayo imepikwa katika Studio ya Silica Music ya Jijini Mwanza chini ya mkono wa Charlee the Best.

“Yaani ni shida pale nitakapoachia hii ngoma; kiukweli ni ngoma ambayo itakuwa ya kipekee na napenda kuwaambia wapenzi na mashabiki wangu ya kwamba wakae mkao wa kula maana ujio ninaokuja nao si wa kitoto, kila kilichofanyika kwenye hii ngoma kimekazwa, yaani ni shidaaa” Alisema Natty wakati akizungumza na Mtanzania Media hii leo.

Mbali na sanaa ya Mziki, Natty E pia ni Mtangazaji wa 99.4 Radio Metro ya Jijini Mwanza ambapo kiukweli amekuwa kivutio kikubwa kwa wasikilizaji ambao wanafuatilia showz zake.

“Kwanza mimi hapo awali nilikuwa sijui kama naweza kuwa Mtangazaji matata kama nilivyo hivi sasa, nakumbuka kuna siku nilipeleka wimbo wangu Radio Metro na nikawa nimepewa Interview, baada ya ile Interview watu walionisikia waliniambia mbali na mziki pia naweza kuwa Mtangazaji” Alisema Natty ambae anakaza vile inavyopaswa katika mziki wa Hip Hop hapa nchini.

Aidha anasema “Hatimae baada ya kushauriwa kuwa naweza kuwa Mtangazaji nilianza kufanya mazoezi ya kutangaza na nakumbuka mwanzo mwa mwakanilisikia tangazo Radio Metro wakihitaji Mtangazaji wa kike na walikuwa wakipokea demo, nami nikaandaa demo nikapeleka na nikabahatika kuingia tatu bora na hatimae kupata nafasi ya kuwa Mtangazaji wa Metro FM, kikukweli nawashukuru wote waliokitambua kipaji changu hususani uongozi wa Metro Fm na wafanyakazi wengine akiwemo Mo.Jay ambae alikuwa Mtangazaji wa Metro FM ambae alinijenga katika tasnia hii ya utangazaji”.

Recommended for you