Audio & Video

“Tuna uwezo wa kufunga kamera hadi chooni CCM Kirumba”- Katibu wa CCM

on

Judith Ferdinand, BMG Habari

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Raymond Mwangwala amewataka wapenzi wa soka kuitunza vyema miundombinu ya uwanja wa soka wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwani ni tegemeo katika michezo mbalimbali Kanda ya Ziwa.

Mwangwala ameyasema hayo wakati akizungumza na BMG na kuongeza kwamba kunapokuwa na mechi, baadhi ya watu wakiwemo mashabiki uharibifu wa miundombinu uwanjani hapo ikiwemo kuiba koki za maji ambapo husababisha bili kubwa ya maji, kutumia karatasi wakati wa kujisaidia haja na kusababisha matundu ya vyoo kuzima.

Alisema uharibifu huo unasababisha gharama kubwa na  kupelekea kila siku kufanya marekebisho hivyo wananchi wanapaswa kulinda miundo mbinu hiyo.

“Tuna uwezo wa kufunga kamera hadi chooni lakini jambo hilo ni siri na siyo vizuri kumuangalia mtu wakati akikidhi haja hivyo ni wajibu wa kila mmoja ni kutunza miundombinu ya uwanja huo na kuwa mlinzi wa mwenzie”. Alibainisha Mwangwala.

Bonyeza HAPA kwa habari zaidi

Recommended for you