Audio & Video

Mjadala wa Wanamabadiliko mkoani Mwanza wapamba moto

on

Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yasin Ally akizungumza kwenye mjadala/ mdahalo wa Wanamabadiliko mkoani Mwanza hii leo.

BMG Habari-Pamoja Daima!

Katika kuelekea Siku ya Wanawake 2018, Shirika la OXFAM kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI limeendesha Mjadala wa Wanamabadiliko mkoani Mwanza ukiangazia Mpango wa serikali kutokomeza Ukatili wa Kijinsia katika kuelekea Uchumi wa Viwanda.

Mjadala huo uliohusisha washiriki kutoka asasi mbalimbali nchini, umefunguliwa na Constansia Gabusa ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 08.03 ya kila mwaka. Fuatilia mjadala huo unaofanyika Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

Mgeni rasmi, Constansia Gabusa ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akifungua mjadala huo.

Recommended for you