Audio & Video

Watanzania kunufaika na mikopo ya maji kutoka benki ya Equity

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Benki ya Equity imetoa semina ya siku mbili kuanzia leo Juni 08, 2018 kwa wakazi wa Jiji la Mwanza kuhusu huduma ya mikopo ya maji safi na usafi wa mazingira inayotolewa na benki hiyo kupitia mradi wa majaribio wa WASH (Water Sanitation and Hygiene).

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji benki hiyo, Betty Kwoko amesema huduma hiyo itawawezesha wananchi, wafanyabiashara pamoja na taasisi mbalimbali kupata huduma za mikopo kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa maji safi pamoja na usafi wa mazingira ikiwemo ujenzi wa vyoo bora.

Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Mhe.Marry Tesha ameipongeza benki ya Equity kwa kutekeleza mradi wa WASH kwani utasaidia wananchi wengi kupata huduma ya maji safi ambapo ametoa wito kwa wananchi kulinda na kutunza vyema miundombinu ya maji.

“Nawaomba sana washiriki wa semina hii muwe mabalozi kwa wananchi wengine, tunapokuta bomba limepasuka tutoe taarifa kwa mamlaka inayohusika na maji MWAUASA ili waweze kurekeisha na kupunguza upotevu wa maji. Yale mabomba ya maji taka sijaona yanapasuka sana lakini naamini likipasuka hilo taarifa itatolewa haraka kutokana na adha yake”. Amesisitiza Mhe.Tesha.

Meneja Mradi wa WASH kutoka benki ya Equity Johanes Msuya amesema kupitia mkopo wa maji, wananchi na taasisi mbalimbali wataweza kuunganishiwa huduma ya maji safi kutoka mamlaka husika za maji, kuboreshewa vyoo na benki itagharamia gharama zote na watakuwa wakilipa mikopo/ gharama hizo kidogo kidogo.

Baada ya Mwanza, wakazi wa mikoa mingine ikiwemo Dar es salaam, Arusha na Mbeya watapatiwa semina hiyo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji benki ya Equity, Betty Kwoko akizungumza kwenye semina hiyo

Meneja Mradi wa WASH kutoka benki ya Equity, Johanes Msuya akizungumza kwenye semina hiyo

Mhandishi Godadi Mgwatu ambaye ni Meneja Udhibiti Ubora wa Maji kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza MWAUASA akiwasilisha mada kwenye semina hiyo.

Mmoa wa washiriki wa semina hiyo akichangia mada

Washiriki wa semina hiyo iliyohusisha wateja wa benki ya Equti, wananchi, wafanyakazi wastaafu, wajasiriamali pamoja na viongozi wa serikali za mitaa.

Washiriki wa semina hiyo

Tazama BMG Online TV hapa chini 

SOMA Benki ya CRDB yasaidia kuboresha huduma za afya na ulinzi Jijini Mwanza

Recommended for you