Audio & Video

Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela atunukiwa cheti cha pongezi

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ALAT tawi la mkoa wa Mwanza imemtunuku cheti pamoja na fedha shilingi laki mbili, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela John Wanga kwa ushiriki wake mzuri katika mikutano ya jumuiya hiyo.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa ALAT wilayani Sengerema, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoani Mwanza Hilal Elisha alisema Mkurugenzi Wanga ameongoza kwa ushiriki wa mikutano miongoni mwa wakurugenzi wa halmashauri zote.

Mkurugenzi Wanga alielekeza fedha alizokabidhiwa zinunue mchele kilo 200 kwa ajili ya wanafunzi wa shule maalumu za msingi Mitindo wilayani Misungwi pamoja na Itumbili wilayani Magu ambapo kila shule itapokea kilo 100.

Mkutano wa ALAT mkoani Mwanza ulifunguliwa na Mkuu wa Wilaya Sengerema Mwl.Emmanuel Kipole kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza ambapo alizitaka halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato badala ya kulalamika kwamba baadhi ya vyanzo vyake ikiwemo kodi ya majengo vimehamishiwa Serikali Kuu.

Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza Hilal Elisha (wa pili kulia) akimkabidhi fedha Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela John Wanga (kushoto) zilizoambatana na cheti cha pongezi.

Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela John Wanga (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi Manispaa ya Misungwi Eliurd Mwaiteleke ili kununua mchele kilo 100 kwa ajili ya wanafunzi wa shule maalum ya msingi Mitindo.

ISOME PIA HABARI HII Halmashauri mkoani Mwanza zatakiwa kubuni vyanzo vipya vya mapato

Recommended for you