Audio & Video

Baadhi ya wazazi wanavyowarubuni watoto wao

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kwa mujibu wa Taasisi ya Taifa ya Takwimu hali ya kiwango cha ukatili wa kijinsia katika mikoa ya Kanda ya Ziwa bado iko juu ambapo takwimu za mwaka 2015/16 zinaonyesha mikoa ya Mara na Shinyanga inaongoza ikiwa na asilimia 78 huku mkoa wa Mwanza ukiwa na asilimia 60.

Ili kupambana na hali hiyo kwa mkoa wa Mwanza, shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI lilianzisha mradi wa majaribio wa kuhamasisha na kuijengea uwezo jamii ili kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wasichana na wanawake katika Kata 10 za wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Akizungumza hii leo kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Idara, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Madiwani, Mahakama, Polisi pamoja na Sungusungu, Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI Yassin Ally amesema mafanikio makubwa yameanza kuonekana kupitia mradi huo.

Mradi huo unaofadhiliwa na shirika la misaada la watu wa Ireland (Irish Aid) ulianza kutekelezwa mwaka jana katika Kata 10 ambazo ni Misungwi, Usagara, Igokelo, Koromije, Idetemya, Mabuki, Misasi, Sumbugu, Mbarika pamoja na Nhundulu na baada ya kuonyesha mafanikio utaanza kutekelezwa katika Kata zote 27 za Halmashauri ya Misungwi.

Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI akifafanua jambo kwa vitendo kwenye mafunzo hayo

PIA SOMA Shirika la KIVULINI lawanoa wanafunzi wilayani Misungwi ili kufichua Ukatili

Recommended for you