Audio & Video

Mkuu wa Wilaya Nyamagana awaonya wanaowaajiri watoto kazi za nyumbani

on

BMG Habari-Pamoja Daima!

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza ameomba yeyote mwenye taarifa za mtoto mdogo kuajiriwa kazi za nyumbani, amfikishie taarifa hizo ili achukue hatua za kisheria.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe.Merry Tesha amepiga marufuku tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuwaajiri watoto wadogo kufanya kazi za nyumbani na kuwanyima haki zao za msingi ikiwemo elimu.

Mhe.Tesha ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mahafali ya kwanza ya wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza, waliohitimu mafunzo ya salon chini ya shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WoteSawa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Aidha Mhe.Tesha amewahimiza wazazi na walezi kuishi vizuri na wafanyakazi wao nyumbani kwa kuwapa elimu na mafunzo mbalimbali huku wakiwa wanafanya kazi badala ya kuua ndoto zao kisa tu ni wafanyakazi wa nyumbani.

Kwa mjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mtoto anatambulika kuwa na umri chini ya miaka 18, ingawa kwa mjibu wa sheria ya kazi  mtoto mwenye umri kuanzia miaka 14 anaruhusiwa kuajiriwa kazi zenye sitaha, ambapo hatua hii inaleta mkanganyiko na baadhi ya watu kuitumia fursa hii vibaya kuwatumikisha watoto.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Jumla ya wafanyakazi 17 wa nyumbani kwa ufadhili wa shirika la WoteSawa, wamehitimu mafunzo ya salon na kukabidhiwa vyeti ambapo shirika hilo chini ya Mkurugenzi wake Angel Benedict linashirikiana na taasisi ya “Novo Foundation” kutekeleza mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani.

Hafla ya mahafali haya imefanyika Machi 07,2018 katika viunga vya ofisi za WoteSawa zilizopo Capripoint Jijini Mwanza, hii pia ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tuimarishe Usawa wa Kijinsia Na Uwezeshaji Wanawake Vijijini”. Bonyeza HAPA kutazama picha zote.

Recommended for you