Audio & Video

Mongella akemea migogoro na rushwa, asisitiza uwajibikaji

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongell amekemea vitendo vya rushwa na migogoro kwenye Halmashauri za mkoa huo huku akisisitiza viongozi na watendaji kuwajibika katika utendaji kazi wao ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Hayo yamesemwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Mwl. Emmanuel Kipole wakati akifungua mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) tawi la Mkoa wa Mwanza uliofanyika jana wilayani Magu.

Kando ya mkutano huo Mhe. Mwl. Kipole akazungumza na BMG Online Tv na kusisitiza juu ya yale aliyoyazungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

Tazama hapa juu BMG Online Tv

Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Mwl. Emmanuel Kipole akifungua mkutano wa ALAT mkoani Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Katibu Tawala wilayani Magu akiwasilisha salamu za Mkuu wa Wilaya hiyo
Katibu wa ALAT mkoani Mwanza, Chrispin Luanda ambaye pia ni Mkurugenzi Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema akifafanua jambo kwenye mkutano huo
Wajumbe wa ALAT mkoani Mwanza

Recommended for you