Habari Picha

Mbunge Mabula ataka mradi wa maji ukamilike kwa wakati

on

Judith Ferdinand, BMG

Mhandisi wa Maji katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza ametakiwa kuhakikisha anasimamia vyema mradi wa maji na usafi wa mazingira vijijini Kahama-Nyamadoke ili kuwaondolea wananchi adha ya kupata maji safi na salama.

Mbunge jimbo la Imelema, Mhe.Dkt.Angeline Mabula alitoa agizo hilo leo wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo.

“Mradi huu ni wa muda mrefu kutokana na hapo awali ufuatiliaji kutotiliwa mkazo lakini awamu hii mradi unapaswa kukamilika ili kuondoa adha iliyopo”. Alisema Dkt.Mabula.

Mhandishi wa maji wilayani Ilemela, Anna Mbawala alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu ambapo  ulishindwa kukamilika Juni 2016 kutokana na changamoto ya kuchelewa kwa fedha za utekelezaji kutoka Serikali Kuu.

“Mradi huu umefikia asilimia 70 na utawanufaisha wakazi 11,867 kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Sangabuye, Kahama, Igombe, Kayenze, Nyafula, Igogwe, Kabusungu, Nyamwilolelwa, Magaka,Wilunya,Lukobe,Ibinza, Bujimile na Nyamadoke.

Recommended for you