Michezo

Mshindi wa Rock City Marathon 2017 aweka mambo hadharani

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Mshindi wa kwanza mashindano ya  Rock City Marathon (2017),  katika mbio za km tatu maalum kwa ajili ya wazee, Christina  Urio (57) mkazi wa Mabatini jijini Mwanza, mewataka wazee kujiwekea utaratibu wa kushiriki  kwenye mashindano kama hiyo ili kuweka mwili katika hali kutopata magonjwa.

Mashindano hayo ambayo yanayoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International  yalifanyika kwa mara ya nane hivi karibuni jijini Mwanza ambapo aliibuka mshindi kwa mara ya tano mfululizo katika mbio hizo.

Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na BMG nyumbani kwake, na kubainisha kwamba siri ya kushinda nafasi ya kwanza kila mwaka katika mashindano hayo ni kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi  mapema.

Urio alisema ni vema wazee kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi  sambamba na kujitokeza  kwa wingi katika michezo na mashindano mbalimbali kama hayo kwani huburudisha na kusaidia  kuepusha magonjwa.

Pia alisema viongozi wanawajibu wa kuwashauri wazee na vijana kufanya mazoezi ili kuepusha  vitendo vya uhalifu, kwani akili na mawazo yatakuyamejikita kwenye mazoezi na kusahau mambo mabaya hasa kwa vijana yakiwemo kuvuta bangi kutumia madawa ya kulevya, kuiba na kufanya mapenzi katika umri mdogo.

Hata hivyo alisema jamii inapaswa kutambua kuwa  michezo haichagui umri wa mtu kwani kuna baadhi ya watu huwacheka wazee pindi wanapofanya mazoezi  kwa kusema kuwa  muda umeshaisha.

“Nasikitika kuona watu wanawacheka wazee, pindi wanapofanya mazoezi na husau kuwa haya chagui rika la mtu bali huepusha  kupatwa na magonjwa yasiyo ambukiza kama kisukari na presha,”alisema Urio.

Recommended for you