Habari Picha

Mtendaji Mkuu NFRA aridhishwa na ubora wa nafaka mkoani Ruvuma

on

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi.Vumilia Zikankuba (katikati) akikagua mahindi wakati wa ununuzi katika kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo mkoani Ruvuma.

Kaimu Afisa Mtendaji NFRA Bi.Vumilia Zikankuba (wa tano kushoto) akisisitiza jambo baada ya kutembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela mkoani koani Ruvuma.

Afisa ubora wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), akikagua mahindi kwenye kituo cha ununuzi cha Kigonsela mkoani Ruvuma. 

Na Mathias Canal, NFRA

Zoezi la kununua nafaka ya mahindi kwa ajili ya akiba ya taifa ya chakula linaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambapo wakulima kwa kiasi kikubwa wameitikia wito uliotolewa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wa kutonunua mahindi yasiyokuwa na ubora.

Hata hivyo baadhi ya maeneo kumeibuka changamoto ya ubora wa mahindi kutokana na changamoto ya mvua za msimu pamoja na jua kali hali iliyosababisha mazao kuharibikia shambani.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu NFRA), Bi.Vumilia Zikankuba ameendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya ununuzi ambapo hivi ambapo Oktoba Mosi, 2018 alitembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo mkoani Ruvuma kukagua mwenendo wa zoezi la ununuzi katika kituo hicho.

Katika ziara hiyo ya Mtendaji Mkuu wa NFRA mkoani Ruvuma ambaye pia ni Meneja wa Kanda ya Songea, Amos Mtafya alieleza kuwa Kanda ya Songea pekee imepangiwa kununua jumla ya tani 7, 000 kwa awamu ya kwanza ya ununuzi na hadi kufikia jana, Kanda hiyo ilikuwa imenunua zaidi ya tani 6,000.

Ili kuimarisha dhana ya Ushirika, Wakala umenunua kwa kiasi kikubwa mahindi kupitia vyama ya Ushirika na vikundi vya wakulima yaani SACCOS na AMCOS ambazo jumla yake ni 23 zilizobainishwa na uongozi wa Mkoa Ruvuma.

Vikundi hivyo vya wakulima ni kutoka katika Halmashauri ya Wilaya Madaba, Songea Vijijini, Mbinga Mji, Mbinga Vijijini,  Namtumbo na Wilaya Nyasa.

Bi. Zikankuba aliridhishwa na hali ya ubora wa nafaka iliyonunuliwa na kuwahimiza watumishi wa NFRA kuendekea kusisitiza na kununua mahindi yenye vigezo vya ubora unaokubalika kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Chakula.

Katika hatua nyingine Bi. Zikankuba aliwapongeza watumishi wa NFRA kwa kazi nzuri ya wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao na wakala kwa ujumla.

Recommended for you