Audio & Video

Mtoto mwenye ulemavu wa macho aliyebarikiwa kipaji kikubwa

on

Jumanne ya Utoaji ama kwa kimombo “Giving Tuesday” ni siku ambayo huadhimishwa kila mwaka duniani katika kila jumanne ya mwisho wa mwezi Novemba, ambapo wanajamii, taasisi na wadau mbalimbali hujitolea kusaidia mahitaji kwa watu wenye uhitaji.

Jumanne ya mwaka huu Novemba 28, wafanyakazi wa shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA, wanawatembelea watoto wenye ulemavu katika shule ya St.Magdalena Wa Canose Igoma Jijini Mwanza na kutoa zawadi na mahitaji mbalimbali.

Hakika watoto hawa wanawapokea wageni wao kwa furaha na kuwaonyesha vipaji vya hali ya juu ikiwemo kipaji cha mtoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona.

Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima kutazama picha!

Recommended for you