Makala

BMG ndani ya kiwanda cha “Mwanza Pure Drinking Water” Jijini Mwanza

on

BMG Habari #PamojaDaima hii leo tumekaribishwa katika kiwanda cha kuzalisha maji ya kunywa “Mwanza Pure Drinking Water”, chini ya kampuni ya kizalendo ya Fide Investments Company Limited kilichopo Nyamhongolo Ilemela Jijini Mwanza.

Tumekutana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo, Frank George Mbwana na kutueleza kwamba kiwanda hicho kilianza uzalishaji mwezi wa 12 mwaka jana na hadi sasa bidhaa zake zinapatikana katika mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Geita pamoja na Kahama mkoani Shinyanga na baadaye Singida na mikoa mingine itafuatia.

Tumeshuhudia uwekezaji wa kisasa kiwandani hapo na kubwa zaidi ni uzalishaji bora wa maji ya kunywa ambayo kila mtanzania anaweza kumudu bei yake ambapo katoni moja ya maji chupa ndogo inauzwa Tsh.3,200 na katoni kubwa inauzwa 7,500.

“Tunatoa fursa kwa mtanzania yeyote kutumia maji ya Mwanza ikizingatiwa hivi sasa Tanzania ni nchi ya viwanda na sisi kwa kufuata kauli mbiu hiyo tumeitekeleza kwa vitendo ili kuendana na kasi ya Mhe.Rais John Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda”. Ameeleza Mbwana.

Tembelea tovuti ya kiwanda hicho www.fideinvestments.co.tz ama kurasa za facebook na Instagram kwa jina la “Mwanza Pure Drinking Water” ama simu 0677 045 801/ 0657 82 70 44 kwa mahitaji ya maji bora ya Mwanza Drinking Water, Fahari ya Ziwa Victoria ambapo kuna maji kuanzia chupa ya ujazo wa nusu lita kwa Tsh.500, lita moja kwa Tsh.800 na lita moja na nusu kwa Tsh.1,000

Tazama BMG Habari, Pamoja Daima habari zaidi.

Recommended for you