Audio & Video

TCRA yakabidhi vifaa vya mawasiliano katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA leo Juni 21, 2018 imekabidhi vifaa mbalimbali vya mawasiliano vyenye thamani ya shilingi Milioni 22 pamoja na kodi, katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza ili kurahisisha huduma za kimawasiliano katika ofisini.

Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo nchini, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba amevitaja vifaa hivyo kubwa ni pamoja na kamera za mbili (picha mnano na nyongevu), redio, kompyuta mpakato (Laptop) na Printa.

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella amesema vitasadia kurahisisha huduma za mawasiliano kulingana na kasi ya Mhe.Rais Dkt.John Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza mamlaka za serikali kuwa mstari wa mbele kwenye utoaji wa taarifa na kwamba pia vitasaidia kurahisisha kazi kwa wanahabari wote mkoani Mwanza.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA nchini, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kushoto) vifaa vya mawasiliano vilivyotolewa na mamlaka hiyo

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA nchini, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kushoto) machapicho kutoka mamlaka hiyo ambayo hutoa elimu kuhusu matumizi salama ya mawasiliano ikiwemo mitandao ya kijamii. Machapisho hayo pia hutolewa bure kwa wananchi

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA nchini, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba akionyesha machapisho ya mamlaka hiyo ambayo hutolewa bure kwa wananchi ili kutoa elimu ya matumizi sahihi ya huduma za kimawasiliano ikiwemo mitandao ya kijamii

Mkurugenzi wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Lawi Odielo akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo. 

SOMA TCRA yasisitiza vyombo vya habari kuzingatia maudhui bora

Recommended for you