Audio & Video

Mwenyekiti wa Bodi Ikungi Sekondari amshukuru DC Ikungi

on

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu ameendelea kupokea pongezi baada ya kuanzisha ligi soka ya “Ikungi Elimu Cup 2017” ili kuhamasisha wananchi wa wadau mbalimbali ili kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu wilayani humo.

Kwenye uzinduzi wa ligi hiyo uliofanyika jumamosi Agosti 19,2017 uwanja wa shule ya sekondari Ikungi, Mhe.Mtaturu alikabidhi mifuko 100 ya simenti na kuungwa mkono na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali waliochangia mifuko 194 na hivyo kusaidia upatikanaji wa mifuko 294 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ikungi ambao ulikwama tangu mwaka 2009.

Siku hiyo pia ulifanyika uzinduzi wa zoezi la kufyatua matofali ambapo Kata zote wilayani Ikungi zimedhamiria kufyatua matofali 10,000 kila Kata ili kusaidia ujenzi wa madarasa, nyumba za waalimu, maabara pamoja na vyoo.

Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima kutazama picha

Recommended for you