Habari Picha

MWILI WA MZEE KOMOTE KUZIKWA LEO WILAYANI TARIME.

on

Mazishi ya marehemu mzee Raphael Chacha Komote (87) yanafanyika hii leo nyumbani kwake Tarime mkoani Mwanza.

Mzee Komote aliyezaliwa Julai Mosi mwaka 1930, alifariki dunia Juni 04,2017 katika hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza  baada ya kuugua kwa muda.

Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu kwa wakazi wa Jiji la Mwanza ilifanyika jana Juni 05,2017 katika kanisa la SDA Mabatini kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani Tarime.

Mchungaji kutoka kanisa SDA akiongoza ibada ya kuuaga mwili wa marehemu, kanisa la SDA Mabatini

Mtoto wa marehemu ambaye pia ni diwani wa Kata ya Nkende, Daniel Komote, akjitoa salamu za shukurani.


Tazama Video hapa chini