Audio & Video

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Mwanza atoa zawadi kwa mashabiki zake

on

Baada ya kimya cha muda, hatimaye mwimbaji wa nyimbo za injili Jijini Mwanza, Elisha Wallace maarufu kama Elisha Wa Upendo amejibu kiu ya mashabiki zake kwa kuachia video mpya.

Ameachia rasmi video hiyo hii leo Disemba 06,2017 ikiwa ni video yake ya kwanza baada ya kufanya vizuri na nyimbo nne ambazo ni Upendo, Ahsante, Nakupa Sifa pamoja na Umenipa Kibali.

Video hiyo ni ya wimbo uitwao Ahsante uliotengenezwa na H.Pol kutoka studio za Pango Records Jijini Mwanza huku video ikitengenezwa na EVP Media kutoka Kenya chini ya mwongozaji Mike.

Hakika Elisha Wallace amefunga vyema mwaka 2017 na video hii ni zawadi tosha kwa mashabiki zake ambapo amesema yuko tayari kwa ajili ya mialiko mbalimbali na anapatikana kupitia nambari 0762 54 78 95 Mwanza.

BMG Habari, Pamoja Daima!

Recommended for you