Audio & Video

UMEISIKIA HII KUHUSU NDONDO CUP 2017 JIJINI MWANZA?

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Mashindano ya Ndondo Cup 2017 yanatarajia kutimua vumbi  Semptemba 20 mwaka huu Jijjni Mwanza.

Ni kwa  mara ya kwanza mashindano hayo kufanyika jijini hapa, ambayo yataunguruma katika uwanja mkongwe na wa kisasa wa Nyamagana, ambapo yatashirikisha timu  16 kutoka wilaya ya Ilemela na Nyamagana.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Katibu  Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza(MZFA) Leonard Malongo alisema, zoezi la kujiandikisha litaanza kesho tarehe 4 semptemba saa 10 jioni kwenye ofisi za chama hicho,ambapo zoezi hilo ni bure wala asitokee dalali wa kuwaomba fedha.

Malongo alisema,dirisha la usajili litafungwa zitakapo kamilika timu 16 zitakazowai kujisajili na gharama ya ushiriki ni 300000.

“Mashindano haya kwa msimu huu, yatashirikisha timu kutoka wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana,na msimu ujao watapanua wigo kwa wilaya nyingine kwani jijini hapa yanafanyika  kwa mara ya kwanza, na tutatumia uwanja mkongwe na wakisasa wa Nyamagana tofauti na Dar es salaam,” alisema Malongo.

Alisema,lengo la mashindano hayo,ni kuwezesha vijana wa mitaani na kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa soka,pia kuwaweka watu pamoja ambao watapata fursa ya kutojihusisha na vitendo viovu.

Pia alisema,kupitia mashindano hayo wanaiunga serikali mkono juu ya vita ya rushwa na madawa ya kulevya kwani vijana watajikita katika kuonyesha vipaji  na wananchi kuvishuhudia.

Aidha alisema, timu zinazotakiwa kushiriki ni zile zenye usajili na za mtaani ambazo zimejiunga pamoja,pia kila timu inaruhusiwa kuwa na wachezaji wasiozidi watatu ambao wameisha cheza ligi za juu kama ligi kuu kwa ajili ya kuleta hamasa kwa wadogo zao na kujifunza mbinu mbalimbali za mchezo huo.

Hata hivyo aliwaomba wadau wa soka waandae timu vizuri ili kuleta hamasa zaidi pamoja na wananchi kujipanga kushangilia kwani kutakua na zawadi kwa kikundi cha ushangiliaji bora.

Kwa upande wa zawadi Malongo alisema, mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha  shilingi  milioni 3 wa pili  milioni 2 wa tatu milioni 1 ,Wa nne  laki 5,huku mchezaji bora,muamuzi bora na kipa bora wataondoka na shilingi laki tano kila mmoja, kwa ajili ya kuleta hamasa uwanjani waandaaji wa mashindano hayo yamepanga kutoa zawadi ya milioni 1 kwa kikundu bora cha ushangiliaji.

Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima kutazama uzinduzi

Recommended for you