Habari Picha

Ndugu wanahabari Msaada wa haraka unahitajika

on

Na Dotto Mwaibale
Ndugu wanahabari mwenzetu Patrick Mwillongo anaumwa na amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Temeke kwa ajili ya matibabu.
 
Mwillongo anasumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu ambao umesababisha ashindwe kujimudu kufanya jambo lolote. Kwa umoja wetu na tabia tuliojijengea kama wanahabari tujitokeze kumsaidia mwenzetu ambaye anapita katika kipindi kigumu.
 
Mwillongo ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea na anafanya shughuli zake katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na awali alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali likiwemo Jambo Leo na yale yanayomilikiwa na Kampuni ya New Habari.
 
Kwa atakayeguswa kumsaidia anaweza kutoa mchango wake kupitia namba M-PESA-0754 36 29 90, Tigo-Pesa ni 0712 72 70 62

Kutoka kushoto ni wanahabari Hellena Mwango, Careen, Kulwa Mwaibale na mke wa Patrick Mwillongo wakiwa wamekaa nje ya jengo la hospitali ya mkoa Temeke wakitafakari namna ya kumsaidia Mwillongo walipofika  kumjulia hali.

Recommended for you