Audio & Video

DC Makete ampongeza Mbunge Viti Maalum CCM mkoani Njombe

on

Mbunge wa Viti Maalum mkoani Njombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Neema Mgaya (kushoto), akimkabidhi DPO Makete, SP. Aloyce Kayera (katika) mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya gereza la Ndulamo. Kulia ni Mkuu wa wilaya Makete mkoani Njombe, Mhe. Veronica Kessy.

Mkuu wa wilaya Makete, Mhe. Veronica Kessy (kulia), akimpongeza mbunge wa Viti Maalum mkoani Njombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Neema Mgaya (kushoto) baada ya kukabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya gereza la Ndulamo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Mhe. Veronica Kessy amemshukuru mbunge wa Viti Maalum mkoani Njombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Neema Mgaya kwa kuitikia ombi lake la kuchangia mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya gereza la Ndulamo wilayani humo.

Akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi mifuko hiyo, Mhe. Kessy amemuomba mbunge huyo kuendelea na ari hiyo katika kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Njombe.

SP. Aloyce Kayera, DPO wilayani Makete amesema ujenzi wa zahanati hiyo unatarajia kuanza hivi karibuni hivyo ametoa rai kwa viongozi na wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kusaidia ujenzi huo ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wafungwa.

Mbunge Mgaya amekuwa kwenye ziara ya kutembelea wilaya zote mkoani Njombe na kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mifuko ya saruji pamoja na mashuka ya wagonjwa katika zahanati, vituo vya afya na pamoja hospitali mkoani humo.

Tazama hapa chini BMG Online Tv

SOMA>>>NJOMBE: Mbunge Neema Mgaya aendelea na ziara, akabidhi saruji na mashuka

Recommended for you