Audio & Video

NJOMBE: Mbunge Neema Mgaya aendelea na ziara, akabidhi saruji na mashuka

on

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Njombe, Mhe. Neema Mgaya amekabidhi msaada wa mashuka katika Vituo vya Afya 10 na Hospitali tatu zilizopo mkoani humo ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo Kibena ambao umegharimu zaidi ya Milioni nne.

Msaada huo ambao umekabidhiwa katika Vituo na Hospitali zenye msongamano mkubwa wa wagonjwa umetajwa kusaidia kumaliza tatizo la upungufu wa mashuka ambapo kwa mujibu wa Dkt. Winfred Kyambile ambaye ni Mganga Mfawidhi mkoani Njombe, inaelezwa kitandanda kinapaswa kuwa na mashuka yasio pungua manne.

Mhe. Mgaya ameeleza kutoa msaada huo kutokana na uhitaji mkubwa wa mashuka uliopo katika Vituo vya Afya na Hospitali mkoani Njombe na kwamba mbali na changamoto ya mashuka serikali ni vyema ikatupia jicho zaidi katika hospitali ya Kibena ambayo inaelezwa haina chumba cha upasuaji, Chumba cha wagonjwa mahututi pamoja na chumba cha kuhifadhi watoto njiti hali ambayo inasababisha kutoa huduma chini ya ubora unaotakiwa.

Dkt. Winfred Kyambile ambaye ni Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Njombe Kibena amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kueleza kwamba baadhi ya changamoto zimeanza kushughurikiwa na serikali ikiwemo ujenzi wa jengo la upasuaji.

Kwa upande wao baadhi ya wagonjwa wakiwemo Oleria Nyagawa na Neema Sanga wamesema msaada uliotolewa na mbunge Mgaya utawasitili kwa kiasi kikubwa huku wakiwataka viongozi wengine kuiga mfabo huo.

Mbali na kutoa mashuka katika Vituo vya Afya na Hospitali zipatazo 13 mkoani Njombe, mbunge huyo pia amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi na ukarabati katika vituo hivyo.

Mifuko hiyo ni zaidi ya tani 10 ambayo inalenga kusaidia ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati ikiwemo Kituo cha Afya Lugawala, Ludewa K pamoja na Zahanati ya Gereza la Ndulamo Makete.

Aidha amekabidhi mashuka takribani 400 katika Zahanati na Vituo vya Afya katika wilaya za Ludewa, Makete, Wanging’ombe na Njombe mkoani Njombe pamoja na Hospitali za wilaya Makete, Ludewa na Njombe ambapo vitu vyote, mifuko ya saruji na mashuka vina thamani ya shilingi Milioni saba.

Tazama hapa chini BMG Online Tv

Recommended for you