Habari Picha

Mwanza watakiwa kuzingatia matumizi bora ya vyoo

on

Judith Ferdinand, BMG

Wananchi mkoani Mwanza wametakiwa kuendeleza utamaduni wa kujenga na kutumia vyoo bora ili kuepukana na maambukizi ya magonjwa ya kuhara yanatokanayo na minyoo ama kichocho.

Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewei kipaumbele, Dkt.Mabai Leonard ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wanahabari na kuongeza kwamba magonjwa ya minyoo na kichocho yanaweza kuambukizwa ikiwa wanajamii hawatazingatia usafi ikiwemo kujisaidia ovyo badala ya kutumia vyoo.

Alisema ugawaji wa dawa pekee hauwezi kumaliza magonjwa hayo hivyo ni vyema jamii ikahakikisha inazingatia kanuni za usafi, kunawa mikono baada ya kutoka chooni, kunawa vyema kabla na baada ya kula pamoja na kuzingatia usafi wa mwili na mazingira.

Na Dkt.Rehman Maggid kutoka mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele alisema zoezi la ugawaji dawa katika ngazi ya jamii linaendelea tangu Agosti 06 hadi 12, 2018 hivyo jamii inapaswa kuhamasika kutumia dawa hizo.

Recommended for you