Habari Picha

PICHA ZA MAHABA ZA MSANII ELIZAYO HB KUTOKA JIJINI MWANZA AKIWA NA VIDEO QUEEN WAKE ZANASWA.

on

Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza (Kulia) akijiselfisha na Agness (Kushoto) ambae ni Video Queen wake alietokelezea katika Video ya Waiting For You. Kuna tetesi kwamba wawili hawa kwa sasa wako katika penzi zito.

Na:Binagi Media Group
Imekuwa ni kawaida kwa Wanamuziki na Waigizaji mbalimbali hususani wa kiume kuanzisha mahusiano na Waigizaji wa Kike au Video Queens wanaokuwa wanafanya nao kazi, na hili limekuwa likitokea si kwa Tanzania tu bali hata nje ya Tanzania.

Sasa iko hivi; baada ya Binagi Media Group kuweka bayana kuwa inapokea matukio ya aina mbalimbali kwa njia ya email na whatsupp (binagimediagroup@gmail.com & 0757 43 26 94), hatimae imepokea picha za mahabati kama zinavyoonekana kutoka kwa chanzo kimoja zikimuonyesha Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza akiwa na Video Queen alietokelezea katika Video yake iitwayo Waiting For You.

Baada ya Mtandao huu kupata picha hizo, ulimtafuta Elizayo kwa njia ya simu na kutaka kujua ukweli wa picha hizo ambazo zinamuonyesha akiwa na Video Queen wake aitwae Agness.

“Sina mahusiano kabisa na Video Queen wangu, hizo picha tulikuwa tukijiselfie kiutani tu baada ya kuwa tumetoka location wakati tunatengeneza video ya Waiting For You na zilianza kusambaa baada ya simu yangu kupotea”. Alisema Elizayo huku akiwatupia Lawama wanaosambaza picha hizo.

Juhudi za kuwatafuta Msanii Elizayo HB na Video Queen wake Agness ili kuongea nao zaidi bado zinaendelea na utapata nafasi ya kuwasikiliza Kupitia Binagi Radio pindi tu watakapopatikana, kwa sasa yetu macho.
BONYEZA PLAY KUTAZAMA VIDEO YA ELIZAYO-WAITING FOR YOU via BINAGI TV

Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza (Kulia) akijiselfisha na Agness (Kushoto) ambae ni Video Queen wake alietokelezea katika Video ya Waiting For You. Kuna tetesi kwamba wawili hawa kwa sasa wako katika penzi zito.
Jamani? Na hii nayo ni ya Utani?
Hapa ni Agness alijiselfieee na Elizayo HB

Recommended for you