Audio & Video

Hoja za papo kwa hapo baina ya Polisi, Madereva na Makondakta

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Chama cha Madereva na Makondakta wa Daladala Mkoa wa Mwanza MWAREDDA kimeeleza kufanikiwa kupambana na makondakta feki ambao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya wizi katika vituo mbalimbali Jijini Mwanza.

Mwenyekiti Msaidizi wa chama hicho, Ezekiel Lameck aliyasema hayo jana kwenye hafla ya kukabidhi kadi za NHIF kwa madereva na makondakta 36 ambao ni wanachama wa MWAREDDA.

Hata hivyo baada ya kauli hiyo, Mkuu wa Kituo cha Polisi Buzuruga Stendi aliwahimiza madereva na makondakta wa chama hicho kuongeza juhudi kwani bado kuna malalamiko ya kuwepo kwa makondakta feki katika vituo mbalimbali hivyo wasisite kuwafichua kwani wao ni rahisi kuwatambua.

PIA SOMA Nyamagana akabidhi Bima za NHIF kwa madereva na Makondakta

Recommended for you