Audio & Video

Rais Magufuli atunukiwa cheti cha pongezi

on

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza hivi karibuni alipofanya ziara ya kikazi mkoani Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) tawi la Mkoa wa Mwanza imemtunuku Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli cheti cha pongezi.

Cheti hicho kimepokelewa jana na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Mwl. Emmanuel Kipoke kwenye mkutano wa ALAT uliofanyika wilayani Magu.

Baada ya kukabidhi cheti hicho, Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza, Hilali Elisha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Magu akazungumza na BMG Online Tv na kueleza sababu za jumuiya hiyo kumtunuku Mhe. Rais Dkt. Magufuli cheti cha pongezi.

Mwenyekiti wa ALAT mkoani Mwanza, Hilali Elisha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Mwl. Emmanuel Kipole (kulia) aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza cheti cha kumpongeza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Tazama BMG Online Tv hapa chini

SOMA Malengo ya wana Bujora kupata shule ya sekondari yatimia

Recommended for you