Audio & Video

Michuano ya Ramadhan Cup 2018 yamalizika kwa kishindo Jijini Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Fainali ya 10 ya michuano ya kombe la Ramadhan Cup mwaka huu 2018 imefikia ukingoni katika kituo cha michezo Mirongo kwa timu ya Uhuru Rangers kuikung’uka timu ya Mirror FC bao 2-0.

Goli la kwanza liliweka wavuni na mchezaji Baraka Kumalija huku Said Malori akihitimisha kwa bao safi la pili na hivyo magoli hayo kuiwezesha timu ya Uhuru Rangers kutwaa kombe la Ramdhan Cup 2018.

Kwa matokeo hayo, timu ya Uhuru Rangers imejishindia mbuzi wawili wa nyama pamoja na kombe huku mshindi wa pili akijishindia mbuzi wa nyama mmoja ambapo Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella aliyekuwa mgeni rasmi alikabidhi zawadi hizo kwa washindi.

Mhe.Mongella alimpongeza mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe.Stanslaus Mabula kwa kudhamini michuano hiyo na kuahidi kwamba michuano ijayo atatoa shilingi laki tano kwa mshindi wa kwanza na shilingili laki mbili kwa mshindi wa pili.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo, Ahmed Misanga alisema michuano ya mwaka huu imefanyika chachu kubwa ya kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana ambapo timu mbalimbali ikiwemo Simba, Yanga na Mbao zilituma wawakilishi wao kutafuta wachezaji.

Mbali na kuendeleza vipaji vya soka, pia michuano ya Ramadhan Cup imekuwa ikifanyika katika kipindi cha mwezi mtukufu ili kuhamasisha upendo, amani, matendo mema na kuwaepusha vijana kujihusisha na makundi maovu.

Michuano hiyo imedhaminiwa na Ofisi ya Mbunge Nyamagana, taasisi ya First Community, UVCCM Kata ya Mirongo pamoja na wadau mbalimbali wa soka.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (kulia), akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Uhuru Rangers (kushoto) baada ya timu yake kuibuka bingwa wa michuano ya Ramadhan Cup 2018 Jijini Mwanza

RC Mongella akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza timu ya Uhuru Rangers

Washindi wa pili, Mirror FC wakipabidhiwa zawadi ya mbuzi wa nyama

Michuano ya Ramadhan Cup 2018 ilikuwa na ushindani mkubwa

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza kwenye fainali ya Ramdhan Cup 2018

Mkuu wa Mkoa akikagua timu kabla ya mechi kuanza

Viongozi na wadau mbalimbali wa soka walijitokeza kwenye fainali hiyo

Mgeni rasmi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Uhuru Rangers

Mgeni rasmi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Mirror Clan

Mgeni rasmi akisaini kitabu cha wageni

Katibu wa UVCCM Kata ya Mirongo ambaye pia alikuwa Katibu wa Ramdhan Cup 2018, Mussa Kifai akisoma taarifa fupi ya michuano hiyo

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Ramadhan Cup 2018, Ahmed Misanga akizungumza wakati wa fainali ya michuano hiyo jana

SOMA Ramadhan Cup yapamba moto Jijini Mwanza

Recommended for you