Audio & Video

Wanafunzi wa CUHAS Jijini Mwanza wamuunga mkono kijana Raphael Swai

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Wanafunzi kutoka Chuo cha Afya CUHAS wameungana pamoja na kijana Raphael Neleson Swai ambaye amesafiri kutoka Jijini Dar es salaam hadi Jijini Mwanza kusherehekea siku yake ya kuzaliwa hii leo Juni 23 pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha “Pamoja Child and Youth Foundation” kilichopo Nyegezi.

Kijana Swai ambaye ni mzaliwa wa Mkuyuni Jijini Mwanza pamoja na Fredirick Francis Umuzigaba ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wanafunzi Madaktari Tanzania tawi la CUHAS wamezungumza na BMG Online TV na kueleza kilichowashawishi kuwatembelea watoto hao. 

SOMA Salamu za Shukurani kutoka BMG

Recommended for you