Audio & Video

MAKABIDHIANO: Mwalimu aliyezawadiwa Milioni Moja na RC Mwanza

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella leo amekabidhi shilingi milioni moja kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kazunzu iliyopo halmashauri ya Buchosa baada ya shule hiyo kufanya vizuri kwenye mitihadi ya darasa la saba kitaifa.

RC Mongella alitoa ahadi hiyo jana kwenye kikao kazi cha viongozi mbalimbali wa elimu mkoani Mwanza, kilichofanyika Chuo cha Ualimu Butimba Jijini Mwanza.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella (wa pili kulia) akimkabidhi zawadi ya Milioni Moja Mkuu wa Shule ya Msingi Kazunzu iliyopo halmashauri ya Buchosa Mwl.Augustine Masesa (wa pili kushoto) baada ya shule yake kufanya vizuri kwenye mitihani ya darasa la saba kifaifa. Wanaoshuhudia ni Afisa Elimu mkoani Mwanza Mwl.Michael Ligola (kulia) na Mwl.Benoh Kagoma (kushoto) kutoka shule ya msingi Kakobe, Buchosa.

Tazama BMG Online TV hapa chini

SOMA Mwalimu aliyezawadiwa milioni moja na RC Mongella aeleza siri ya mafanikio

Recommended for you