Habari Picha

MAZISHI YA SUGUTA: John Heche ashindwa kuzuia hisia zake

on

BMG Habari-Pamoja Daima!

Mwili wa Suguta Heche ambaye ni mdogo wake na mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini mkoani Mara (Chadema) John Heche umezikwa jana Mei 03, 2018 katika Kijiji cha Nyabhitocho Sirari wilayani Tarime.

Ilidaiwa usiku wa kuamkia April 27, 2018 Suguta alifariki baada ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali (kisu) akiwa mikononi mwa polisi baada ya kukamatwa akiwa bar ambapo jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Tarime Rorya lilikiri kumshikiria askari wake kuhusiana na tukio hilo.

Akizungumza kwenye mazishi hayo, Mbunge Heche alisema familia haiko tayari kupokea fidia ya aina yoyote kutokana na tukio hilo kwani fidia hiyo haitaweza kuurejesha uhai wa mdogo wake na kutaka vitendo vya aina hiyo kukoma si tu wilayani Tarime bali kote nchini.

“Tunachohitaji ni haki na yule aliyetenda tendo hili hatua zichukuliwe juu yake. Mimi nasema kwa uchungu mkubwa kweli kweli, kamanda wangu huyu, mdogo wangu na rafiki yangu amelala hapo mimi namuona, nimeumia kwa kiwango ambacho sijawahi kuumia. Nataka tu niwahakikishie wananchi wa Tarime, na hata wakiniua mimi songeni mbele kutafuta haki”. Alisema Heche.

Suguta Heche alizaliwa mwaka 1990 ambapo hadi mauti yanamkuta alikuwa na miaka 28 na alikuwa bado hajaoa. BMG Habari inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huu.

 

John Heche (mwenye shati jeupe), wanafamilia pamoja na waombolezaji mbalimbali.

Wanafamilia, viongozi wa Chadema pamoja na waombolezaji mbalimbali.

Recommended for you