Audio & Video

Wanahabari waliopata ajali wapokea salamu za Rais kwa hisia kali

on

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa waandishi wa habari pamoja na watu wengine waliopata ajali katika msafara wake uliokuwa ukielekea Ukerewe Septemba 04, 2018.

Salamu hizo zimewasilishwa leo Septemba 07, 2018 na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella na kuongeza kwamba Mhe. Rais Magufuli anatambua mchango wa wanahabari hivyo ameguswa na ajali hiyo.

Wakizungumza kwa hisia kali, baadhi ya wanahabari wamemshukuru Mhe. Rais kwa salamu zake.

SOMA Ziara ya Rais Magufuli mkoani Mwanza

Recommended for you