Audio & Video

Serikali yaahidi kuboresha zaidi huduma za Afya Hospitali ya Rufaa Bugando

on

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema serikali itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando iliyopo Jijini Mwanza kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya hospitalini hapo.

Waziri Mwalimu ametoa kauli hiyo hii leo Januari 26,2018 wakati akizindua mashine ya uchunguzi ya CT-Scan katika hospitali hiyo, iliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni fedha za ndani mapato ya ndani ya hospitali.

Waziri Ummy Mwalimu akizungumza kwenye uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando, Dr.Abel Makubi akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo.

Askofu Flavian Kasala akitoa salamu za Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa Bugando.

Mtaalamu wa tiba ya mionzi Hospitali ya Rufaa Bugando akizungumza kwa ufupi kuhusiana na tiba ya saratani hospitalini hapo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella (katikat), Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza Dr.Leonard Subi (kulia) pamoja na Askofu Flavian Kasala (kushoto) wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo.

Mhe.Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mashine ya CT SCAN katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando Dr.Abel Makubi, Mganga Mkuu mkoa wa Mwanza Dr.Leonard Subi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella na kulia ni Askofu Flavian Kasalaa aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa Bugando.

Recommended for you