Habari Picha

SERIKALI YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SHULE BINAFSI

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Serikali imetakiwa kuendelea kushirikiana na  shule binafsi,ili waendelee kutoa elimu bora kwa vijana ambao ni viongozi wa baadae.

Hayo yamesemwa na Msimamizi wa Shule ya Msingi Lumala English Medium kutoka Shirika la Mabinti wa Maria Sister Yulitha Bura wakati wa uzinduzi wa jengo la utawala na madarasa la shule hiyo,lililogarimu zaidi ya milioni 600.

St.Bura alisema, mabinti wa maria wanatoa huduma kwa kushirikian na serikali, kwani wao wanawasaidia kutoa elimu na malezi bora kwa vijana ikiwemo ya kidini.

Pia alisema, kwa niaba ya shirika hilo anaishikuru serikali kwa kuwapa kibali cha kujenga shule hiyo ya msingi,hivyo anaiomba kuendelea kuwakagua na kuwapa kanuni ambazo inazitaka wafanye ili kupeleka mbele gurudumu la elimu nchini.

Aidha alisema, shule hiyo inalengo la watoto kupatiwa malezi bora na kuwa na maadili mema kwa ustawi wa taifa.

Hata hivyo, aliwashukuru kwa michango na juhudi walizoonyesha katika kukamilisha ujenzi huo,hivyo aliwaomba waendelee kujitoa na kwa wengine ili kuhakikisha taifa linakua na elimu bora.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa uzinduzi huo Padri Alfred Lwamba alisema, ni wakati wa kusaidia vijana na watoto kupata elimu, ili nao waje wawasaidie watoto wao baadae kwani elimu ni uhai na kila kitu maana ata maandiko yanasema itafute sana elimu usiache ikaenda zake.

Kadhalika alisema, wanataka kutoa elimu kwa watoto tena bora kwani wakisoma katika mazingira mazuri husaidia kufaulu na kufanya vizuri kwenye masomo yake.

Recommended for you