Audio & Video

Wafanyabiashara haramu ya Nzige watoweka wilayani Misungwi

on

Mkuu wa wilaya Misungwi, Mhe. Juma Sweda akizungumza kwenye kilele cha kampeni ya kupambana na ukatili wa kijinsia wilayani Misungwi.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi, Fredrick Nyoka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kampeni hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, ACP. Jonathan Shanna akiwasilisha salamu zake kwenye kilele cha kampeni hiyo.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Mhe. Juma Sweda akivishwa shuka la Sungusungu Kata ya Nhundulu wilayani Misungwi.
Mmoja wa Sungusungu wilayani Misungwi akitoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Juma Sweda kwa juhudi zake za kupambana na ukatili wa kijinsia hususani mimba za utotoni na mauaji ya wanawake.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Mhe. Juma Sweda (kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi, Antony Bahebe cheti maalum kutoka shirika la KIVULINI kama ishara ya kutambua mchango wake katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Mhe. Juma Sweda (kushoto), akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi, Fredrick Nyoka cheti maalum kutoka shirika la KIVULINI kama ishara ya kutambua mchango wake katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Mhe. Juma Sweda (kushoto), akimkabidhi Afisa Maendeleo ya Jamii Misungwi cheti maalum kutoka shirika la KIVULINI kama ishara ya kutambua mchango wake katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Burudani kwenye kilele cha kampeni hiyo
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Baadhi ya wanawake maarufu kwa jina la Nzige waliokuwa wanafanya biashara haramu ya kujiuza katika msimu wa mavuno katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, wametoweka baada ya kukosa wateja (wanaume) kufuatia kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia iliyoendeshwa wilayani humo.

Hayo yalibainishwa juzi katika Kaya ya Nhundulu wilayani Misungwi wakati wa kufunga kampeni hiyo iliyodumu kwa kipindi cha wiki nane ambayo imeendeshwa katika Kata 22 kati ya 27 za Wilayani hiyo, iliyolenga kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Mkurugenzi shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema kampeni hiyo imewafikia wananchi 33,420 na kuleta matokeo chanya ikiwemo matumizi sahihi ya kipato msimu wa mavuno ambapo sasa wanafamilia wanatumia vyema fedha hizo ikiwemo kujenga nyumba bora, kununua magodoro ya kisasa badala ya yale ya nyasi maarufu kama Dodoma Ngubalu huku kwa mara ya kwanza biashara haramu ya Nzige katika maeneo mbalimbali kama Kidarajani ikitoweka kutokana na elimu iliyotolewa kupitia midahalo ya wazi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa kampeni hiyo, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi, Fredrick Nyoka alisema imesaidia kupunguza vitendo vya ukatili katika jamii ikiwemo ubakaji, mimba za utotoni pamoja na matumizi mabaya ya fedha msimu wa mavuno na kwamba wananchi wamejengewa utayari wa kuripoti vitendo hivyo pindi vinapotokea.

Kufuatia mafanikio hayo, Mkuu wa Wilaya Misungwi Mhe. Juma Sweda ambaye alikuwa mgeni kwenye kilele cha kampeni hiyo, alitoa rai iwe endelevu ili kuzifikia Kata zote wilayani humo huku akionya kuwashughulikia wale wote ambao hawataacha kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

“…Nitakuwa mkali kuliko pilipili, nitakuwa silali usiku na mchana kufuatilia wale ambao wanaendelea na ukatili…wale wote wasiopenda kutenda haki wajue sasa watapambana na mkono wa mwanaume wa shoka ambaye ni mimi katika mkoa wa Mwanza…”. Alionya Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza ACP. Jonathan Shanna.

Kampeni hiyo ilizinduliwa Julai 04, 2018 na kuendeshwa na Halmashauri ya Wilaya Misungwi kwa ushirikiano wa karibu na shirika la kutetea haki za wasichana/ watoto na wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza.

Tazama BMG Online Tv haoa chini

SOMA>>>Kampeni ya kutokomeza Ukatili Misungwi yahitimishwa kwa mafanikio

Recommended for you