Habari Picha

Shirika la KIVULINI lasaidia uanzishwaji wa Kiwanda katika shule ya Wasichana Bwiru Jijini Mwanza

on

Dakika chache zijazo (sasa ni saa tano majira ya Afrika Mashariki), utafanyika uzinduzi wa kiwanda kidogo cha ushonaji katika shule ya Wasichana Bwiru iliyopo Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Lengo ni kuwajengea ujuzi wanafunzi wa shule hii ili hata wakihitimu masomo yao, wawe na uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali za kiujasiriamali na kujipatia kipato.

Hadi sasa wanafunzi wa shule hii wana ujuzi wa ushonaji nguo na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni ambapo soko kubwa kwa sasa ni kuuziana wenyewe shuleni hapo.

Shirika la kutetea haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza, limeunga mkono kufanikiwa kwa malengo haya.

Baadhi ya vyerehani vilivyotolewa na Shirika la Kivulini.

Wanafunzi hawa wa kidato cha tano na sita wameifa kwenye suala la ufundi stadi

Baadhi ya mavazi yanayoshonwa na wanafunzi wa shule ya Wasichana Bwiru.

Baadhi ya bidhaa ikiwemo sabuni za maji, gundi pamoja na rangi za viatu zinazotengenezwa na wanafunzi wa shule ya Wasichana Bwiru.

 

Recommended for you