Audio & Video

Shirika la KIVULINI lawanoa wanafunzi wilayani Misungwi ili kufichua Ukatili

on

BMG Habari-Pamoja Daima!

Wanafunzi wa shule za sekondari katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wameendelea kujengewa uwezo wa kutambua na kuripoti vitendo vya ukatili majumbani na mashuleni ikiwemo ubakaji vinavyosababisha mimba za utotoni na hivyo kukatisha masomo yao.

Shirika la Kutetea Haki za Wasichana na Wanawake KIVULINI lenye makazi yake Jijini Mwanza, limechukua hatua hiyo kupitia Mradi wake wa Kuhamasisha na Kuijengea Uwezo jamii ili kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wasichana na wanawake wilayani humo.

Akizungumza jana kwenye mdahalo wa wazi uliofanyika katika shule ya sekondari Igokelo, Magreth Kaduela ambaye ni Afisa Mradi kutoka shirika la KIVULINI alibainisha kwamba mradi huo unatekelezwa katika Kata 10 za wilaya ya Misungwi huku pia ukihusisha wanajamii.

Ezekiel Kishosha pamoja na Zawadi Daniel ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Igokelo ambao ni mfano bora wa namna elimu inayotolewa na shirika la KIVULINI inavyobadili fikra za wanafunzi kuhusu vitendo vya ukatili katika jamii na hivyo kuomba elimu hiyo kuendelea kutolewa.

Wanawake na watoto wamekuwa wahanga wakubwa wa ukatili katika jamii hivyo ni wakati mwafaka kuungana pamoja kama wanajamii na kufichua aina zote za ukatili ili tuwe na jamii salama.

Magreth Kaduela ambaye ni Afisa Mradi kutoka shirika la KIVULINI akizungumza kwenye mdahalo huo.

Mmoja wa wanafunzi wa shuke ya Igokelo akichangia mada kwenye mdahalo huo.

Midahalo ya aina hii inafanyika katika Kata mbalimbali wilayani Misungwi.

Bonyeza HAPA kutazama kusoma na picha zaidi.

Recommended for you