Habari Picha

Shirika la Maperece laendeleza vita dhidi ya ukatili kwa wazee

on

Picha kutoka maktaba

Na Oscar Mihayo, Mwanza

Kutokanana kukithiri kwa vitendo vya mauaji ya wazee katika Kata ya Koromije wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, shirika lisilokuwa la kiserikali la kutetea haki za wazee la Maperece limeendesha semina kwa washauri wa kisheria ili kuhakikisha wazee kama tunu ya taifa wanaishi hawakumbani na ukatili katika jamii.

Akizungumza wakati wa utoaji wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Shirika hilo Julius Mwengela alisema semina hiyo ni utekelezaji wa mradi mpya wa kukuza sauti ya jamii utayarishaji na uwajibikaji wa serikali katika kulinda na kutetea haki za wazee na watu wenye ualibino.

Alisema mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa kuzia ukatili dhidi ya wazee unaotekelezwa katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza pamoja na Chato mkoani Geita ambapo unalenga kuwafikia wazee zaidi ya 29,000.

Mwengella alisema mafunzo ambayo wanayotoa ni pamoja na elimu kwa mabaraza ya wazee juu ya haki za wazee, washauri wa koo na familia, elimu ya ndoa na sheria ya aridhi ya mwaka 1999 lakini pia mbinu za kujikwamua na wimbi la umasikini.

“Tunaimani baada ya kuhakikisha elimu hii inasambaa vitendo vya mauwaji kwa wazee na watu wenye ualibino vitakomeshwa kwani chanzo kikubwa cha mambo haya ni mila potofu, imani za kishirikina na umasikini,” alisema Mwengella.

Awali akifunga mafunzo hayo diwani wa Kata ya Koromije, Bilarimini Hilary alisema tangu aingie madarakani mwaka 2010 hadi sasa kila mwaka kati ya wazee watano hadi nane walikuwa wakiuwawa na watu wasiojulikana.

Diwani huyo alitoa wito kwa mashirika mblai mbali kuiga mfano wa Maperece kwani wamejikita katika kuhakikisha kwamba haki ya wazee inapatikana na pia mafunzo muhimu ya kuepuka mila zilizopitwa na wakati.

Kwa upande wake mshauri wa Sheria Agnes Malongo alisema walikuwa wakiishi kwa wasiwasi kutokana na maisha yao kuwa hatarini kutokana na umri wao.

“Sisi tunatuhumiwa kuwa ni wachawi lakini uchawi wenyewe hatuhujui lakini wanaofanya haya ni vijana wetu ambao wanatuuwa ili kurithi Mali” alisema Agnes.

Mtendaji wa kata ya koromije, Elizabeth Banabas,alisema kata hiyo imeweka mikakati maalum kwa ajili ya kuounguza mauaji ya wazee na watu wenye ualibino ikiwa ni pamoja na swala hilo la mauaji kupewa kipau mbele katika kila mkutano.

“Hapa tuliamua kuunda kamati za ulinzi katika kila kijiji na zina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha kwamba ulinzi,amani na usalama vyote vinadhumishwa,” alisema mtendaji.

Recommended for you