Habari Picha

Shirika la Under The Same Sun lataka mabadiliko ya sheria kupambana na ukatili kwa wenye ualibino

on

Judith Ferdinand, Mwanza

Imeelezwa kuwa kutokana na vitendo vya kikatili vinavyoendelea nchini dhidi ya watu wenye ualbino, ipo haja ya kufanyia marekebisho baadhi ya sheria hili kunusuru kundi hilo.

Hii ni kutokana na kuwepo kwa sheria nchini ambazo hazijaelezea endapo kutatokea mtu akamfanyia vitendo vya ukatili mtu mwenye ualbino hatua ipi inatakiwa kuchukuliwa pamoja na adhabu gani inayomstahili kulingana na kosa.

Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi wa Shirika la Under the Same Sun, Vicky Ntetema katika warsha ya mpango wa mafunzo ya uhamasishaji wa fursa sawa za ajira na uelewa wa mifumo ya elimu, sheria za kazi,Haki za binadamu na haki  za ajira kwa watu wenye ualbino, iliyoandaliwa na shirika hilo  ambayo inafanyika kwa siku nne jijini Mwanza.

Ntetema alisema kuna Sheria nyingi ambazo wao kama watetezi wa haki za binadamu wangependa zirekebishwe, ikiwemo sheria ya usafirishaji haramu wa viungo vya binadamu kwa kuongeza vipengele vinavyohusu watu wenye ualbino.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Pia alisema sheria ya tiba asili na mbadala haielezei vigezo ambavyo mtoa tiba anatakiwa kuwa navyo ili apatiwe leseni na badala yake inaelekeza vitu anavyotakiwa kutumia wakati wa kutoa tiba ikiwemo mimea na wanyama ambapo binadamu wapo kundi la wanyama, hivyo baadhi yao utumia mwanya huo kuwafanyia watu wenye ualbino vitendo vya kikatili ikiwemo kuwakata nywele zao.

 

Hivyo alisema ni wakati wa tume ya haki za binadamu, wanasheria, serikali na wadau mbalimbali wakutane na kujadili pamoja na kutoa mapendekezo ya takayofanyika katika kufanyia marekebisho sheria hizo, zinazoonekana  kuwapatia mwanya baadhi ya watu ambao siyo waadilifu ya kuwafanyia vitendo vya kikatili watu wenye ualbino.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Shirika la Under The Same Sun, Maduhu William alisema kuna haja ya kufanyia marekebisho baadhi ya sheria ambazo zinawanyima fursa za kupata haki zao za msingi kisheria watu wenye ualbino ikiwemo Sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ambayo aimlazimishi mwanandoa kwenda kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya mwenza wake,hivyo ikitokea baba amemfanyia ukatili mtoto au mtu  mwenye ualbino, mama atashindwa kutoa ushahidi na kupelekea aliyefanyiwa ukatili kutopatiwa haki yake.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Pia alisema Sheria ya  uchawi ya mwaka 1928, Sheria ya tiba asili na mbadala ya mwaka 2002, Sheria ya ushahidi ya mwaka 2002 na sheria ya  kanuni ya adhabu ni miongoni mwa sheria zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho kulingana na mazingira ili watu wenye ualbino waweze kuishi kwa amani  sambamba na kukomesha ukatili huo.

Hata hivyo Maduhu alimuomba Rais John Magufuli asimamie jambo hilo la kufanyia marekebisho Sheria, I’ll haweze kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati wa viwanda, kwani hawezi kufanikiwa ikiwa wananchi wake hawataki kutoa nguvu kujishughulisha na badala yake wamejikita kwenye imani potofu za kuamini kuwa kufanikiwa mpaka wapate viungo vya watu wenye ualbino.

Recommended for you