Habari Picha

SHIRIKA LA WOTESAWA LAWAUSIA WAZAZI NA WALEZI MKOANI MWANZA.

on

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand,Mwanza
Wazazi na walezi  hasa  walio vijijini wameombwa kutimiza wajibu wao kwakuwapatia watoto mahitaji muhimu, nakuacha tabia ya  kuwatafutia kazi za majumbani.

Hii ni kutokana na uelewa mdogo kwa jamii hasa ya vijijini ya kumchukukia mtoto kama mtumwa,hivyo kushindwa kumpatia mahitaji muhimu na badala yake kumpeleka mjini kufanya kazi za ndani ili kujikimu kimaisha.

Hayo yalisemwa jana na  Ofisa Mtathimini na Ufuatiliaji   wa Shirika la Wote Sawa linalojishughulisha na kutetea haki za watoto  wafanyakazi wa nyumbani   Elisha David, wakati akizungumza na BMG ofisinikwake jijini Mwanza.

David alisema, kutokuepo na umakini wa wazazi katika makuzi na na malezi pamoja na ulevi hasa vijijini hivyo kushindwa kuwahudumia watoto mahitaji muhimu ikiwemo kuwapeleka shule ndio chanzo cha kuwa na watoto wafanyakazi wa ndani.

Pia alisema,ni wajibu wa wazazi kuhakikisha watoto wanapata mahitaji muhimu, ili kutatua changamoto ya ongezeko la watoto wafanyakazi majumbani,hali itakayasaidia kuepuka vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya waajiri.

Hata hivyo alisema, shirika hilo limeweza kutoa mafunzo kwa watoto wafanyakazi majumbani ya haki na wajibu wao,yatakayosaidia kujitambua na kujua nini cha kufanya endapo atafanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo kunyimwa mshahara pamoja na kuanzisha mabaraza ya wafanyakazi wa ndani  watoto kutoka kata 8 mkoani Mwanza.

“Sisi kama  Wote Sawa tunatoa elimu kwawafanyakazi wa ndani, ili waweze kutambuahaki zao za msingi  na kupewa mikataba nawaajiri wao,  kwa kufanyahivyo  kutasaidia  kulinda masilahiyao,”alisema David.

Aidha alisema, ili kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto hao,wamewajengea uwezo viongozi wa serikali za mitaa kwa kufanya majukumu yao na kuwabaini watoto wafanyakazi wa ndani,pamoja na kuwaelimisha jamii ya zaidi ya watu 5000.

Kadhalika aliwaomba viongozi wa kamati za ulinzi na usalama vijijini wasimamie na kuhakikisha watoto wanapelekwa shule.

Vilevile aliwataka watoto waone umuhimu wa kuendelea na shule na kuacha kukimbilia mjini kufanya kazi za ndani.

Aliongeza kwa  kuwataka waajiri wawatambue watoto hao,kama mmoja wa familia na watimize wajibu wao kwa kuwalipa mishahara pia waangalie namna ya kuwapa mahitaji kama watoto wao ikiwemo elimu.

Recommended for you