Audio & Video

SHIRIKA LA WOTESWA LAWANOA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA

on

George Binagi-GB Pazzo

Mratibu wa Shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa majumbani WOTESAWA, Cecilia Nyangasi (pichani juu) amesema shirika hilo limejiwekea mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha kwamba watoto chini ya umri wa miaka 18 hawaajiriwi kufanya kazi za nyumbani hapa nchini.

Nyangasi ameyasema hayo hii leo kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari Jijini Mwanza, yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kusaidia kufikisha elimu katika jamii ili kuondokana na mazoea ya kuwaajiri watoto kufanya kazi za nyumbani na hivyo kuwakosefa fursa mbalimbali ikiwemo kupata elimu.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuwanusuru watoto wafanyakazi wa majumbani na ukatili ikiwemo wa kingono pamoja na kiuchumi ambapo baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi bila malipo ama kwa malipo kidogo.

Aidha ametoa rai kwa serikali kuboresha sheria zinazomlinda mtoto ili kuondoa mkanganyiko ambapo zinamtaja kwamba mtoto ni mwenye umri chini ya miaka 18 lakini bado zinamruhusu kuajiriwa kufanya kazi za nyumbani na kwamba shirika hilo lingependa kuona sheria zinaboreshwa ili kuzuia mtoto chini ya miaka 18 kuajiriwa kwenye kazi mbalimbali ikiwemo za nyumbani.

Nyangasi amebainisha kwamba mwaka jana shirika la WoteSawa lilifanya utafiti katika Kata nne za Jiji la Mwanza ambazo ni Igogo, Mkuyuni, Butimba na Capriont na kubaini kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na utumikishwaji na ili kupambana na hali hiyo shirika hilo lilianzisha mkakati wa kuwafikia watoto waajiriwa, waajiri wao pamoja na viongozi wa serikali za mitaa na kuwaelimisha.

Nao waandishi wa habari, Moses Mathew kutoka gazeti la Daily News pamoja na Rhoby Magira kutoka Redio Afya wamebainisha kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuandika habari na makala zinazoielimisha jamii ili kuondokana na mazoea ya kuwatumikisha watoto kupitia ajira za majumbani.

Itakumbuka kwamba mtoto mfanyakazi wa nyumbani analindwa na sheria kadhaa ikiwemo sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009, sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2017, waraka wa mishahara wa mwaka 2013 pamoja na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa upande wa waraka wa mishahara wa mwaka 2013, mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni ingwa waraka huo hautaji mwajiriwa huyo anapaswa asiwe mtoto.

Mratibu wa WoteSawa, Cecilia Nyangasi akizungumza kwenye mafunzo hayo ambapo kwa pamoja waandishi wa habari Jijini Mwanza wameanzisha ushirikiano mwema katika kutetea haki za watoto wafanyakazi wa majumbani
Shirika la WoteSawa pia limekuwa likiwasaidia watoto wafanyakazi wa majumbani kupata stahiki zao kwa mjibu wa sheria ikiwemo kuwahimiza waajiri kutoa mikataba ya ajira.
Mkufunzi Dotto Bulendu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostino cha Jijini Mwanza, akisisitiza wanahabari kuungana pamoja katika kuibua na kuandika habari/ makala zenye kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani
Afisa Habari shirika la WoteSawa akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mwanahabari Moses Mathew kutoka gazeti Daily News akichangia mada kwenye mafunzo hayo
Mwanahabari Nashon Kenned kutoka gazeti Habari Leo Daily News akichangia mada kwenye mafunzo hayo
Mwanahabari Michael Obunde kutoka TBC Daily News akichangia mada kwenye mafunzo hayo
Mkufunzi Dotto Bulendu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostino cha Jijini Mwanza, akiongoza mjadadala kwenye mafunzo hayo
Wanahabari Jijini Mwanza
Mmoja wa wafanyakazi wa WoteSawa akifuatilia kwa umakini mafunzo hayo
Bonyeza BMG Habari, Pamoja Daima wakisaini mikataba

Recommended for you