Makala

SHIUMA ni suluhisho la sintofahamu baina ya machinga na serikali

on

Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA), Ernest Matondo.

Na Blandina Aristides, Mwanza

Miongoni mwa mambo  ambayo yamekua yakiumiza vichwa viongozi wa serikali nchini ni pamoja na suala zima la wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Machinga waliopo katikati ya miji.

Na hii imetokana na kuwepo na wimbi kubwa la wafanyabiashara hao katika maeneo mbalimbali yasiyo rasimi  na watu  hawa wamekua wakitegemea shughuli hizo  kujipatia kipato kwaajili ya famili.

Nidhahili kuwa, watu hawa wanaonekana kama wavunjifu wa mani kutokana na kukosa chombo cha kuwatetea na kuwasimamia katika utekelezaji wa shughuli zao ya kila siku na wakati mwingine kuonekana kama wasabishaji wa vurungu.

Ni ukweli usio pingika kuwa Halimashauri zimekua zikichangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa vurugu za wafanyabiashara hao, pale wanapotoa maelekezo kwa jeshi la polisi kuwaondoa katika maeneo yao ya kazi bila kuelekeza ni wapi wanatakiwa kwenda kwaajili ya shughuli zao.

Kutokea kwa vurungu  hizo za machinga katika maeneo mbalimbali nchini, kumewafanya  baadhi ya watu  kuwabeza na kuwaona wao kama wavunjifu wa amani kila kukicha jambo ambalo kwa namna moja ama nyingin inaonesha kuwa mtazamo huo hauna mantiki.

Kumekua na matukio mbalimbali ya kuhuzunisha na kustajabisha  kama vile vifo, ulemavu kutokana na vurugu za hapa na pale zisizokuwa na maana lakini pia imepelekea baadhi ya machinga kuachana na biashara hiyo na hayimaye kujiingiza  katika uvutaji wa madawa ya kulevya  japo kwa asilimia kubwa serikali ya awamu ya tano imelidhibiti hilo.

Mkoa wa Mwanza ni miongni mwa mikoa nchini ambao kwa sehemu kubwa umekuwa ukikumbwa na janga hili la wafanyabiashara wadogowadogo kupigwa, kunyang’anywa biashara zao, kufukuzwa katika maeneo yao ya kazi  na wengine kuuwawa bila sababu ya msingi.

Kutokana na hali hiyo, kumekua na jitihada mbalimbali za kuhakikisha watu hao wanafanya biashara zao kwa amani na utulivu lakini pi wanakua na maeneo ya kudumu kwaajili ya shughuli zao za kiuchumia.

Jambo hilo limekua na mlolongo mrefu ambao haukupata majibu na suluhisho mapema  la nini kifanyike, badala yake  vurugu  zimekua zikijirudia mala kwa mala huku machinga hao wakifukuzwa  katika maeneo yao ya  kazi na wakati mwingine kunyang’anywa mali kwa nguvu.

Ernest Matondo ni Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA)ambaye anaeleza kuwa, kupitia shirika hilo upo uwezekano mkubwa wa kuhakikisha vurugu hizo hazitatokea tena kutokana na jitihada zinazofanywa na shirika katika kuwapigania machinga nchini.

SHIUMA ni chombo ambacho kimeanzishwa mwaka 2010 mkoani Mwanza kikiwa na lengo la  kutetea wafanyabiashara waodowadogo maarufu kama Machinga katika wilaya ya Nyamagana na baadaye kulipandisha hadhi na kufanya kazi ngazi ya Mkoa.

Kutokana na shirika hilo kuendelea kufanya kazi kwa weledi mkoani Mwanza, mwaka  2014 shirika hilo lilisajiliwa Kitaifa baada ya kuona machinga nchini nzima hawana chombo cha kuwatetea hususani  pale wanapokutana na changamoto mbalimbali katika shughuli zao za kila siku.

“Lengo  kuu  zaidi lililotufanya kusajili shirika hili nchi nzima  ni kuwaunganisha machinga na serikali kuwa na Umoja lakini pia  kuondoa migogoro isiyo ya lazima iliyokuwepo kati ya serikali na machinga” alisema Matondo.

Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa, usajili huo utaweza  kusaidia kwa asilimia 80 kuondoa  tatizo hilo la vurugu za machinga kwani taklibani  mikoa 13 tayali wamekwisha jiunga katika shirika hilo na tayali wamekwisha pata viongozi watakao ongoza mikoa hiyo na kwamba  mpaka sasa lina zaidi ya wanachama 10,000.

“Usajili wa shirika hili mpaka sasa hivi  umekamilika vizuri nahii ni kutokana na kuwepo na kiongozi  makini tuliyenaye wa Tanzania Rais wetu  John Pombe Magufuli anayejari watu wanyonge na walio na hali ya  chini.

Matondo anaeleza kwamba Rais aliyepo madarakani kwa sasa ni kiongozi ambaye anapaswa kukumbukwa kwa asilimia miamoja na hususani kwa watu wa hali ya chini ambao amekua akiwatetea kwa kila hali bila kujali dini wala kabila la mtu.

Uwepo wake  ni tunu tosha kwa Watanzania, hivyo haina haja ya kumbeza na kutafuta kashifa zisizo na maana  kwani mchango wake ni mkubwa katika kuhakikisha Shirika hili linapata nafasi ya kuwa watetezi wa wafanyabiashara wadogo nchini.

Novemba 2 mwaka 2016 Uongozi wa mkoa wa Mwanza kupitia Mkuu wa mkoa John Mongera na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Marry Tesha ulitoa agizo la kuondolewa kwa machinga katikati ya jiji la Mwanza, jambo ambalo kwa haraka jeshi la polisi lilitekeleza agizo hilo na kuwaondoa malamoja.

Kuondolewa kwa machinga hao kulileta taharuki  kwa wananchi wa Mwanza lakini pia jambo hilo halikumfuhisha Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanislaus Mabula na hivyo kuchukua hatua ya kushughurikia  jambo hilo ili kwa kila namna ili machinga hao wawe na uhuru katika biashara zao.

Hata hivyo shirika la SHIUMA halikua nyuma katika kuwatetea machinga kwani walikua mstari wa mbele kwa kupaza sauti kupitia chombo hicho kwani  walipambana kwa hali na mali ili na kuomba machinga hao wafanye kazi kwa muda wakati wanatafutiwa maeneo mazuri ya kudumu.

Tarehe 6 mwezi Novemba mwaka 2016 Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli  kupitia vyombo vya habari vya Radio na Televihseni alitoa agizo la machinga hao kurudi mjini malamoja na kuwataka waendelee na biashara zao   kama kawaida huku utaratubu maalumu ukifanyika wa kuwapatia maeneo maalumu kwaajili ya biashara zao.

Maelekezo hayo yanaonekana kuzaa matunda kwani  mpaka sasa Serikali kupitia shirika la SHIUMA wapo katika hatua ya mwisho kwaajili ya kupata maeneo ya kudumu lakini pia kufanya usajili wa machinga wote nchini kwaajili ya kupewa vitamburisho maalumu vya kazi ambacho kitamtamburisha kama machinga  lakini pia wawe na maeneo ambayo  atalipia kodi kulingana na kipato chake.

“ Kwa utaratibu utakao kuwepo wa kuwatambua machinga, ni vema kila mtu ashughulikie usajili lakini pia kupata kitamburisho chake na asiyekuwa nacho  atakua hana cha kujitetea hivyo atajikimbiza mwenyewe mjini kwani hatakua na mtetezi wake” alisema.

Katibu wa Shirika hilo Nchini Venatus Anatoryl naye  anaeleza kuwa  SHIUMA imejipanga kufanya kazi kwa weledi lakini pia kuwapigania machinga kote nchi kwa kila namna ili tu kuepukana na vurugu za hapa napale kati ya wananchi na serikali yao.

Mpaka sasa wapo katika mazungumzo ya  kupendekeza maeneo watakapo pangiwa machinga  katika kila mkoa huku akiamini kuwa muda si mrefu machinga watakua katika hali nzuri kwani serikali iliyopo madarakani inawajali na kuwathamini wajasiliamali.

Shiuma inatarijia kufanya  mkutano mkuu utakao fanyika mwezi  Mei mwaka huu ukiwashirikisha viongozi wa Shirika hilo katika mikoa yote ya Tanzania kwaajili ya mazungumzo ya kina kati yao na Serikali ili kujua nini  kifanyike ili suala la machinga lipatiwe ufumbuzi mapema.

“Nia na madhumuni makuu ya Serikali ya awamu ya tano na Shiuma ni  kuhakikisha kila machinga analipa kodi kulingana na biashara yake aliyonayo na tunaimani watakaa vizuri nah ii hali ya ugomvi haitakuwepo tena” alisema.

Anatoryl  anafafanua kuwa  kinacho hitajika zaidi katika mchakato huo ni kuondoa  dhana ya machinga kupigizana kelele na serikali bali washirikiane na serikali wasiwe watu wa vurugu bali wawe watu wa mfano katik nchi za Afrika Mashariki.

Wilium Joseph ni mmoja wa machinga jijini hapa ambaye anaeleza kuwa uwepo wa shirika hilo katika mkoa wa Mwanza umekua ni msaada mkubwa kwa vijana hususani ambao walikua hawana kazi za maana  za kuwapatia kipato cha kutosha.

Aneleza kuwa kupitia mpira wa miguu shirika liliweza kumtambua na hatimaye kumfanya awe kijana mchapazai  baada ya kupewa eneo la kufanyia biashara zake lakini pia hata kwa ushauri na hatimaye kumfanya awe mahali ambapo hakutegemea.

“Mimi nilikua mvuta bangi, mlevi lakini nashukuru sana shirika la Shiuma kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kunisaidia katika maisha yangu mpaka hapa nilipo, nina maisha yangu mazuri na pia wamenifanya mpaka nikwa na mke nawashukuru sana”alisema Wilium.

Inaonekana dhahiri dhana hii ya kuanzishwa kwa  shirika hilo, kuna uwezekano mkubwa wa Machinga kuwa na mazingira mazuri ya kazi zao endapo kutakuwa na ushirikiano wa kutosha kutoka serikalini na wadau wengine wa maendeleo ya nchi.

ZISOME PIA HABARI HIZI MACHINGA MWANZA WAKUBALIANA NA SERIKALI 

MACHINGA, MFUPA ULIOISHINDIKA HALMASHAURI YA JIJI MWANZA

Recommended for you