Makala

SHUHUDIA TUKIO LA KUPATWA KWA MWEZI 2017

on

BMG Habari, Pamoja Daima!

Leo jumatatu Agosti 07,2017 mabara mbalimbali katika sayari ya dunia ikiwemo Afrika yatashuhudia tukio la asili la kupatwa kwa Mwezi ambapo sayari hii ya Dunia itakuwa kwenye mstari mmoja kati ya jua na mwezi.

Hili ni tukio muhimu linalotarajiwa kufuatiliwa na watu wengi hata hapa nchini kwani wamekuwa wakilisoma kwenye vitabu na machapisho mbalimbali bila kujionea uhalisia wake kwa macho hivyo linapotokea huwa ni wasaa mzuri kwa kila mmoja kulishuhudia kwa macho.

Inasadikika kwamba mwaka huu kupatwa kwa Jua kutaonekana kwenye mataifa mengi zaidi duniani na kwamba nchi za Afrika Mashariki zitalishuhudia kwa uzuri zaidi bila hata kuhitaji vifaa vya kitaalmu (majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki), ingawa itakuwa tofauti kwa bara la Amerika ambako tukio hilo halitaonekana kiurahisi.

Tukio jingine ambalo huvutia wengi duniani (ingawa halitokei leo) ni lile la Kupatwa kwa Jua (solar eclipse) ambalo ni tukio la Jua kutoonekana ama kuonekana kisehemu kidogo tu angani wakati wa mchana.

Hutokea wakati Mwezi unapita kati ya Jua na Dunia na hivyo kufunika Jua. Matokeo yake ni kupungua kwa Jua hadi kutoonekana tena hadi kufikia hali ya giza wakati wa mchana. Tukio hili hutokea kwa dakika chache tu.

Kupatwa kwa Jua kunatokea kama dunia, mwezi na jua zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua.

Imeandaliwa na BMG kwa msaada wa mitandao mbalimbali

Recommended for you