Habari Picha

SHULE YA WASICHANA WAJA GEITA YAWAZAWADIA WALIOFANYA VIZURI MASOMO YA SAYANSI KIDATO CHA SITA

on

Gari mbili aina ya IST yenye thamani ya  shilingi milioni 22 yakiwa yamepakiwa nje ya shule hiyo yakisubiliwa kukabidhiwa kwa wanafunzi hao.
Mwanafunzi ambaye amezwadiwa gari Edina Davis ambaye katika matokeo ya kitaifa alishika nafasi ya Tisa  akijaribia gari yake.
Mgeni Rasmi ambaye yupo katika Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi ,Teknolojia na Ufundi Profesa Simon Msanjila akikata utepe kwaajili ya kuwakabidhi magari wanafunzi hao.
Mwanafunzi Bihera Kabaruka ambaye alikuwa mshindi wa pili kati ya wanafunzi kumi ambao wamefanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa kidato cha Sita.
Mkurugenzi wa Shule binafsi za WAJA zilizopo Mkoani Geita Mhandisi  Chacha Wambura  akiwakilisha taarifa ya shule hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi ,Teknolojia na Ufundi Profesa Simon Msanjila.

Na Joel Maduka

Mkurugenzi wa Shule binafsi za WAJA zilizopo Mkoani Geita Mhandisi  Chacha Wambura amewazawadia magari mawili wanafunzi wa kike  waliohitumu Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya wasichana WAJA waliotajwa kufanya vizuri katika masomo ya Sayansii kwenye matokeo ya kidato cha Sita mwaka huu.

Akikabidhi magari hayo mawili  aina ya IST yenye thamani ya  shilingi milioni 22, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Simon Msanjila  amewataka wanafunzi wengine kuiga mfano wa washindi hao na kuzitaka taasisi nyingine pia kuiga mfano uliooneshwa na Bw.Chacha

Mmoja wa wanafunzi waliozawadiwa  ni  Edina Davis ambaye katika matokeo ya kitaifa alishika nafasi ya Tisa amesema  kufanya kwake vizuri na kupatiwa zawadi ya gari kunatokana na kujituma ili kuipata zawadi ambayo imekuwa ahadi ya Mkurugenzi wa shule hiyo kwa wanafunzi wote kuwa angewapatia magari washindi

Recommended for you